Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Sudan Kusini: Mashirika ya kiraia yataka Salva Kiir na Riek Machar wajiuzulu

Mashirika kadhaa - yanayojumuisha wasomi, wanasheria, mashirika ya wanawake na vijana - yametoa wito kwa raia wa Sudan Kusini kuandamana Jumatatu, Agosti 30, kote nchini. Wanamshutumu rais na makamu wa rais kwa kuitumbukiza nchi hiyo katika machafuko.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na makamu wake, kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar (klia) huko Juba, Februari 20, 2020 katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na makamu wake, kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar (klia) huko Juba, Februari 20, 2020 katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Miaka kumi baada ya uhuru wake, Sudan Kusini ni moja wapo ya nchi masikini zaidi duniani. Asilimia 82 ya raia wake wanaishi chini ya kiwango cha umaskini kulingana na Benki ya Dunia, licha ya mafuta na misaada kutoka kwa jamii ya kimataifa.

Sababu kuu za kudorora kwa uchumi wa nchi hiyo ni vita, ukosefu wa usalama, ufisadi ... na uhasama kati ya viongozi wawili: rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar. “Wanapotawala pamoja, hakuna kinachoendelea! Hawakubaliani kwa chochote, ni mvutano tupu. Na wasipokuwa pamoja, vita vinazuka na wanawajibika kwa mateso, uharibifu, na vifo vingi vya raia, ”amebaini Rajab Mohandis moja yamiungano ya mashirika ya kiraia. “Mikataba kadhaa ya amani ilisainiwa kati ya wawili hao, kila wakati wanaahidi kufanya kazi pamoja, na kila wakati mikataba hii inasahaulika. Kutokubaliana kwao kulianza  tangu vita vya kupigania Uhuru na hali hii inaendelea hadi leo, ”ameongeza.

"Kuna raia wengi wa Sudan Kusini ambao wanaweza kutawala nchi hii vizuri zaidi kuliko wao"

Miaka mitatu baada ya makubaliano ya mwisho ya amani yaliyosainiwa mnamo 2018 (na ambayo bado hayajatekelezwa kikamilifu), hali ya kisiasa imekumbwa tena kizungumkuti, mashirika ya kiraia yamebaini. Mashirika haya yanawashutumu viongozi hao wawili kwa kuweka mbele masilahi yao ya kibinafsi kabla yamasilahi ya nchi. “Rais Salva Kiir anaogopa kuondolewa madarakani, na hivyo kutumia wakati wake kujaribu kukaa madarakani kwa gharama ya nchi. Kwa kuongezea, wote wawili wanafahamu kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu umefanywa, na kwamba siku hawatakuwa tena amadarakani, wanaweza kufikishwa mahakamani. Wasudan wengi wa Kusini wanaweza kuendesha nchi hii bora zaidi kuliko wao. Ni wakati wa kubadilika; kwa sababu viongozi wetu wameshindwa na hatuwezi kuendelea hivi. "

Mashirika tofauti kwa hivyo yanataka maandamano kudai kujiuzulu kwa viongozi hao wawili.

Serikali haijajibu, lakini msemaji wa rais ameonya juu ya kile anachokiita "tamko la vita", akikumbusha kwamba makubaliano ya amani yanabaini wazi kwamba uchaguzi utafanyika mnamo mwaka wa 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.