Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UHURU

Matukio muhimu yaliyotokea katika miaka 10 ya Uhuru wa Sudan Kusini

Sudan Kusini inapoadhimisha miaka 10 ya uhuru wake, Julai 9, tunathathmini baadhi ya  matukio muhimu yaliyotokea ndani ya kipindi hicho katika taifa hilo changa duniani ambalo limeshuhudia vita ambavyo vimesababisha maafa ya watu 380,000.

Wananchi wa Sudan Kusini walivyosherehekea uhuru wao Julai 09  2011
Wananchi wa Sudan Kusini walivyosherehekea uhuru wao Julai 09 2011 Roberto SCHMIDT AFP/File
Matangazo ya kibiashara

2011 Kuundwa kwa taifa jipya

Tarehe 9 Julai, mwaka 2011, Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka kwa Sudan, baada ya kuanza kujitegemea  kwa miezi miaka sita na vita vya zaidi ya miaka 20.

Salva Kiir amekuwa rais wa nchi hiyo, huku Riek Machar akiwa Makamu wake. Wawili hao walikuwa katika vuguvugu la kupigania uhuru wa nchi hiyo SPLM.

Kiir anatokea kabila la Dinka. Machar, kabila la Nuer.

Robo tatu ya nchi hiyo ina mafuta hasa jimbo la Abyei, lakini nchi jirani ya Sudan inatumiwa kupitisha bomba linalosafirisha mafuta hayo.

 

2012 Mzozo wa mafuta

Kati ya mwezi Machi na Mei, mataifa ya Sudan Kusini na Sudan yalizua mapigano kuhusu mmiliki halali wa maeneo yenye utajiri wa mafuta katika êneo la Heglig.

Mji wa Heglig upo mpakani kati ya nchi hizo mbili, katika jimbo la Kordofan nchini Sudan na Unity nchini Sudan Kusini.

Jeshi la Sudan Kusini lilipiga kambi kwa muda katika eneo hilo kabla ya kuondoka.

Sudan Kusini pia ilisitisha uzalishaji wa mafuta kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa madai kuwa, jirani yake Sudan alikuwa anaiba rasilimali hiyo.

 

2013 Kuzuka kwa vita

Julai 23, rais Kiir alimfuta kazi Makamu wake Machar na Mawaziri pamoja na wasaidizi wao. Makamanda wakuu wa polisi pia waliachishwa kazi.

Machar alimshtumu Kiir kwa tabia za kidikteta baada ya tukio hilo.

Usiku wa Disemba 16, kulizuka mapigano makali jijini Juba, kati ya vikosi vinavyomuunga mkono rais Kiir na Machar.

Kiir alidai kuwa Machar alijaribu kumpindua kutoka madarakani, madai ambayo yalikanushwa na Machar.

 

2016: Machar akimbilia uhamishoni

Baada ya miaka mitatu ya mapigano, Machar na Kiir walitia saini mkataba wa amani, na Machar akarejeshwa tena katika nafasi ya Makamu wa rais.

Machar alirejea jijini Juba Aprili 26, 2016 na kuapishwa katika nafasi hiyo.

Ilipofika mwezi Julai, mapigano yalizuka tena na Machar akaamua kuikimbia tena nchi akidai Kiir alikuwa analenga kumuua.

 

2018: Mkataba wa amani

Kiir na Machar walikutana kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili Juni 20.

Septemba 12, wawili hao walitia saini mkatba mpya wa amani, kumaliza vita ambavyo vilikuwa vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 380,000 na wengine zaidi ya Milioni nne kusalia wakimbizi.

Mkataba huo, uliwezesha kuundwa kwa serikali ya muungano, ambayo ilianza kufanya kazi Machi 2020 huku Machar akiwa tena Makamu wa rais.

 

2020: Utekelezwaji wa mkataba wa amani

Licha ya mkataba wa amani kutekelezwa, makundi yenye silaha yaliendelea kupigana.

Umoja wa Mataifa, uliongeza muda wa vikosi vyake vya kulinda amani kuendelea kuwa nchini humo, huku ikizuia uingizwaji wa silaha nchini humo.

Juni, 2020 Kiir na Machar walikubaliana kuhusu usimamizi wa majimbo.

 

2021: Onyo la Umoja wa Mataifa  

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwezi Aprili, ilionya kuhusu utekelezwaji wa mkataba wa amani ambao, ulikuwa ukifanyika taratibu na hivyo, kutishia nchi hiyo kurejea kwenye vita.

Rasimu ya katiba mpya, imeanza kuandikwa lakini kuliunganisha vikosi mbalimbali kuwa jeshi moja, bado ni changamoto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.