Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Wapinzani na wanadiplomasia walengwa na udukuzi Rwanda

Wanyarwanda zaidi ya 3,500 huenda wamekuwa wakidukuliwa na kampuni ya masuala ya ujasusi wa mtandao kutoka nchini Israel, NSO Group kwa mujibu wa uchunguzi wa vyombo vya Habari za vya Kimataifa.

Paul Kagame, raiw wa Rwanda, katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 2008 huko Geneva.
Paul Kagame, raiw wa Rwanda, katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 2008 huko Geneva. AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watu waliokuwa wanadukuliwa kwa mujibu wa uchunguzi huo, ni simu ya mkononi ya Carine Kanimba, binti wa mwanaharakati na mpinzani wa rais Paul Kagame, Paul Rusesabagina.

Imebainika kuwa, simu yake ilidukuliwa mara kadhaa tangu mwezi Januari mwaka huu kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International.

Binti huyo wa Rusesabagina, amelaani hatua hiyo wakati huu, wakiwa kwenye harakati za kuhakikisha kuwa baba yake aliyefunguliwa mashtaka ya ugaidi, anakuwa huru.

Aidha, Kanimba, mwenye umri wa miaka 28, raia pacha wa Marekani na Ubelgiji, amesema inasikitisha kuwa baada ya kumteka na kumtesa baba yake, mazungumzo yake ya simu na afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelji Sophie Wilmes na Mawakili wake, yalikuwa yanasikilizwa.

Licha ya shutuma hizi, kampuni hiyo ya Israeli ya NSO, inasema mtandao huo unanuiwa kupambana na ugaidi na makosa mengine ya jinai  wala sio kusikiliza mawasiliano ya wananchi wa mataifa mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.