DRC na Rwanda zakubaliana kuhusu masuala ya usalama na uchumi
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, zimekubaliana kushirikiana kwenye maeneo matatu yenye umuhimu kati ya nchi hizo jirani.
Imechapishwa:
Haya yamejiri baada ya kikao kati ya rais Felix Tshisekedi, na mwenzake Paul Kagame waliokutana mjini Goma siku ya Jumamosi.
Mikataba hiyo inahusu nchi hizo mbili kushirikiana na kulinda miradi ya uwekezaji, kukomeshwa kwa utozwaji kodi mara mbili kwa bidhaa zinazovuka kati ya nchi hizo mbili na ushirikiano wa kampuni za Aurifère du Kivu, Maniema (SAKIMA SA) na DITHER LTD.
Mbali na makubaliano hayo ya kiuchumi, viongozi hao pia wamekubaliana kushirikiana kwenye masuala ya usalama Mashariki mwa DRC, ili kuwezesha mazingira mazuri ya kufanikisha shughuli za maendeleo.
Viongozi hao wawili waliokutana mjini Rubavu upande wa Rwanda siku ya Ijumaa, kuthathmini madhara yaliyojitokeza kutokana na mlipuko wa Volkano, siku ya Jumamosi, walitembelea eneo la Kibati, katika mkoa wa Kivu Kaskazini pia kuthathmini madhara yaliyojitokeza baada ya mlipuko huo.