Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Museveni aapa kuwaangamiza wahalifu baada ya shambulio dhidi ya maafisa wake

Rais wa Uganda Yoweri Musevei ameapa kuwashinda watu waliomshambulia Waziri wa Kazi na uchukuzi na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenereali Katumba Wamala kwa lengo la kumuua.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. via REUTERS - PRESIDENTIAL PRESS SERVICE
Matangazo ya kibiashara

Museveni amewaita washambulizi hao wasiojulikana kuwa ngururuwe, wasiothamini maisha.

Shambulizi hilo lilifanyika jana asubuhi na watu wasiojulikana jijini Kampala na kusababisha kifo cha binti wa Waziri huyo na dereva wake waliokuwa kwenye gari.

Hii sio mara ya kwanza kwa watu mashuhuri kulengwa na kuuawa lakini hakuna ukamataji wowote na washukiwa kupelekwa Mahakamani ambao umewahi kushuhudiwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.