Pata taarifa kuu
UGANDA-CORONA

Uganda yakana rais Museveni kupokea chanjo ya Covid- 19

Waziri wa Afya nchini Uganda, Jane Aceng, amekunusha taarifa ya rais Yoweri Museveni, na maafisa wengine wakuu serikalini wamepewa chanjo ya virusi vya corona kisiri na  mapema kabla ya taifa hilo kupokea chanjo.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa amevalia barakoa wakati wa uchaguzi. Hapa ilikuwa tarehe 14 / 01 / 2021
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa amevalia barakoa wakati wa uchaguzi. Hapa ilikuwa tarehe 14 / 01 / 2021 Badru Katumba AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kauli yake inajiri baada ya gazeti la Daily Monitor nchini humo, na lile la Marekani la Wall Street Journal, kuchapisha taarifa kwamba maafisa wa ngazi ya juu serikalini wakiongozwa na rais Museveni, tayari wamepokea chanjo ya virusi vya corona, hata kabla ya chanjo ya virusi hivyo kuwasili nchini Uganda.

Nataka kusema kuwa rais Museveni, wala washirika wake wa karibu hawajapokea chanjo ya virusi vya corona

 amesema waziri Aceng.

Hadi kufikia sasa Uganda imesajili visa 40,221 vya maambukizi ya corona.

Uganda inatarajia kupata dozi 100,000 ya chanjo ya virusi vya corona aina ya AstraZenaca, kutoka India, na nyingine dozi 300,000 aina ya Sinapharm kutoka China.

Serikali hata hivyo haijatangaza ni lini chanjo hizo zitawasili nchini Uganda.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.