Pata taarifa kuu
UGANDA-MATOKEO

Museveni atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ametangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika siku ya Alhamisi kwa kupata ushindi wa asilimia asilimia 58.6 dhidi ya  mpinzani wake wa karibu Bobi Wine aliyepata asilia 34.8.

Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni, alitangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 14 2021
Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni, alitangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 14 2021 GAEL GRILHOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Jaji Simon Mugenyi Byabakama amemtangaza Museveni mshindi wa Uchaguzi huo na sasa ataendelea kuwa madarakani kwa muhula wa sita.

“Tume ya Uchaguzi inamtangaza Yoweri Museveni kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Uganda,” alisema Jaji Byabakama.

Bobi Wine tayari amesema hatambui matokeo hayo, na hata kabla ya matokeo kutangazwa siku ya Ijumaa alidai kuibiwa kura.

Wanajeshi wamezingira makaazi yake kutoka siku ya Ijumaa kwa kile wanachosema ni kumpa ulinzi.

Uchaguzi nchini Uganda umefanyika kwa mazingira magumu, kufuatia kufungwa kwa mitandao ya kijamii na Internet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.