Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Museveni kutawazwa kwa muhula wa sita kama rais wa Uganda

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anaapishwa leo kuendelea kuongoza taifa hilo la Afrika Mashariki mwa muhula wa sita.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. AP - John Muchucha
Matangazo ya kibiashara

Museveni mwenye umri wa miaka 76, anaendelea kuwa madarakani baada ya kutangazwa mshindi wa Uchaguezi wa urais uliofanyika mwezi Januari na kutangazwa kuwa alishinda kwa asilimia 58 dhidi ya mpinznai wake Bobi WIne, mwanasiasa kijana.

Kuelekea kuapishwa kwa Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35, usalama umeimarishwa jijini Kampala.

Wageni zaidi ya Elfu nne watahudhuria sherehe hizo za kumwapishwa Museveni wakiwemo maraia saba kutoka mataifa ya Afrika.

Maafisa wa usalama wametoa onyo kali kwa wapinzani kuwa wasijaribu kuleta vurugu wakati wa kuapishwa kwa Museveni wakat hu baadhi ya wafuasi wa upinzani wakikamatwa na kuzuiwa/

Chama cha Bobi Wine NUP kimeendelea kudai kuwa rais Museveni alkiiba kura na kuwataka wafuasi wake kutumlia siku hii kwa kufunga na kuiombea nchi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.