Pata taarifa kuu
UFARANSA-JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Oparesheni maalumu ya kupokonya silaha makundi ya wapiganaji yaanza nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Jeshi la ufaransa lililopelekwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hii leo jumatatu litaanzisha operesheni maalum ya kupokonya silaha makundi yote ya wapiganaji wanaoendelea kuuzorotesha usalama nchini humo. Hayo yanajiri wakati waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius akisema kuwa watu takribani mia nne wameuawa hadi kufika hapo jana, akaongeza kuwa uhasama wa kidini umeendelea kukita mizizi na kusababisha mauaji makubwa.

REUTERS/Hippolyte Donossio
Matangazo ya kibiashara

Raisi wa Senegal Macky Sall ameonya kuwepo na mchango maalumu wa umoja wa Ulaya pamoja na ule wa Umoja wa Afrika katika kuisaidia serikali ya Ufaransa kuukamilisha uwezo wake wa kutoa msaada wa dharura pale ambapo utahitajika.

Wachambuzi wa masuala ya Kisiasa wanahisi kuwa hatua ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha ziada cha wanajeshi wa Ufaransa huko Bangui, kutarahisisha harakati za kurejesha amani katika maeneo yenye migogoro.

Idadi ya wanajeshi wanaounda Kikosi cha Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati imefikia elfu moja na mia sita, wengi baadhi yao wamelekwa huko Bossangoa na vile vile Jijini Bangui baada ya kutokea Mauaji ya wananchi wengi Huko Jamhuri ya Afrika Ya Kati.

Hali ya usalama imeendelea kuwa tete tangu kuangushwa kwa utawala wa Rais aliyepinduliwa mwezi Machi mwaka huu Francois Bozize.

Waasi wa Seleka ambao walifanikisha mapinduzi hayo bado wameendelea kuwa tishio kwa usalama licha ya Rais Djotodia kutangaza kulivunja kundi hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.