Pata taarifa kuu
KENYA-ICC

Mahakama ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Mkenya anayetuhumiwa kuwahonga Mashahidi ili wajitoe kwenye kesi

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa zamani raia wa Kenya Walter Osapiri Barasa akituhumiwa kuwa sehemuya mtandao unaofanya kazi ya kujaribu kuwahonga mashahidi wa kesi inayomkabili Naibu Rais William Samoei Arap Ruto wajitoea. Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ICC Fatou Bensouda ndiye ametangaza hatua ya kutolewa kwa hati hiyo ya kukamwata Baraza ambaye anatajwa kuwa kinara wa kuongoza mtandao huo wa kuwahonga mashahidi ili wajiondoe na hatimaye kesi inyomkabili Naibu Rais Ruto isiwe na nguvu.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa ICC Fatou Bensouda ndiye ametangaza kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Walter Barasa
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa ICC Fatou Bensouda ndiye ametangaza kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Walter Barasa AFP / Daniels Evert -Jan
Matangazo ya kibiashara

Bensouda ametoa wito kwa Serikali ya Kenya kumkamata mara moja Barasa na kumfikisha The Hague ili aweze kukabiliana na makosa ya uhalifu wa kivita yanayomkabili kwani amekuwa sehemu ya kutaka kuharibi mchakato mzima wa kutolewa ushahidi unaondelea kwa sasa.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Bensouda amesema hati hiyo ya kukamatwa ilitolewa tarehe 2 ya mwezi Agosti lakini kwa muda wote huo Mahakama haikuwa imetaka suala hilo litambulike na umma hadi leo ilipotoa idhini ya kutangazwa rasmi.

Mahakama ya ICC inamtuhumu Barasa kwa kutaka kuwahonga mashahidi watatu jumla ya shilingi milioni 1.4 za Kenya ili wajiondoe kwenye orodha ya mashahidi ambao wanapaswa kueleza kile kilichotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Tayari Barasa amejitokeza na kukanusha madai yote yaliyoelekezwa kwake na kusema ni vitu ambavyo vimepangwa kwani yeye hajawahi hata kukutana na Naibu Rais Ruto kwa lengo la kuandaa mpango huo wa kuwahonga mashahidi ili wajiondoe.

Barasa amesema hii ni mara ya kwanza kwa Mahakama ya ICC kutoa hati ya kukamatwa mtu anayetuhumiwa kuwatisha mashahidi ili wasiweze kutoa ushahidi mbele ya Mahakama hiyo kitu ambacho kinadhihirisha ni suala la kupanga.

Mwandishi huyo wa Habari wa zamani anatajwa kufanya kazi katika kampuni ya Rais Uhuru Muigai Kenyatta inayotambulika kwa jina la Mediamax kabla hajaacha kazi na ndiyo maana amewekwa kwenye mtandao wa naibu Rais Ruto.

Naibu Rais Ruto amerejea huko The Hague kwa ajili ya kusikiliza mashtaka yanayomkabili baada ya kupewa juma moja la mapumziko ili aweze kushiriki kipindi cha majinzi baada ya kushambuliwa kwa Jumba la Biashara la Westgate.

Jaji Kiongozi kwenye kesi inayomkabili Naibu Rais Ruto na Mwandishi wa Habari Joshua Arap Sang, Chile Eboe-Osuji ameamuru kesi hiyo kuendelea hadi mwezi ujao na kusisitiza mashtaka hayo yatakuwa yanasikilizwa hadi jumamosi kufidia muda uliopotea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.