Pata taarifa kuu
USALAMA-MAPIGANO

Scholz: Armenia na Azerbaijan zimekubaniana kutotumia vurugu kutatua tofauti zao

Armenia na Azerbaijan zimejitolea kusuluhisha tofauti zao "kwa amani na bila kutumia vurugu," Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Jumamosi baada ya mkutano na viongozi wa nchi hizo mbili hasimu za Caucasia (Caucasus).

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashini na Rais wa Azerbaijani Ilham Aliev hawajaarifu kuhusu mazungumzo wanayofanya mjini Munich ambapo mkutano huu wa kila mwaka ni tukio la mazungumzo mengi ya kidiplomasia kuhusu mizozo ya sasa.
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashini na Rais wa Azerbaijani Ilham Aliev hawajaarifu kuhusu mazungumzo wanayofanya mjini Munich ambapo mkutano huu wa kila mwaka ni tukio la mazungumzo mengi ya kidiplomasia kuhusu mizozo ya sasa. © Gavriil Grigorov & Ukrainian Presidential Press Office, AP - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Olaf Scholz "amekaribisha kwa uwazi ahadi iliyotolewa leo na pande zote mbili za kutatua tofauti zilizopo za maoni na masuala yaliyosalia kwa njia ya amani pekee na bila kutumia vurugu," imesema taarifa kutoka kwa baraza la mawaziri mwishoni mwa mkutano huu, kando ya Mkutano wa Usalama wa Munich, na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliev na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachini.

Wawili hao hawajaarifu kuhusu mazungumzo wanayofanya mjini Munich ambapo mkutano huu wa kila mwaka ni tukio la mazungumzo mengi ya kidiplomasia kuhusu mizozo ya sasa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na Nikol Pashinian huko Munich, ambaye amesikitishwa na "awamu mpya ya mvutano kati ya Armenia na Azerbaijan," kulingana na ripoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Urushianaji risasi kwenye mpaka

Armenia na Azerbaijan zilishtumiana siku ya Jumanne kwa urushianaji risasi kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, karibu na Nerkin Hand (kusini mashariki mwa Armenia), tukio ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Armenia kulingana na Yerevan. Wakati huo huo, Nikol Pashinian aliishutumu Azerbaijan siku ya Alhamisi kwa kutaka "vita kamili" na Armenia. Rais Aliev, kwa upande wake, aliyechaguliwa tena kwa muhula wa 5, alitangaza siku ya Jumatano katika hotuba yake ya kuapishwa kuwa hataki tena upatanishi wa kimataifa katika masuala ya Caucasus.

Mizozo ya mipaka imesababisha nchi hizo mbili kuwa vitani kwa miaka mingi. Mnamo mwezi wa Septemba 2023, jeshi la Azerbajani, kupitia shambulio kubwa, lilichukua udhibiti kamili wa Nagorno-Karabakh, eneo la milimani ambalo lilikuwa limepoteza tangu kuanguka kwa USSR, na kusababisha makumi ya maelfu ya wakaazi kukimbilia Armenia.

Tangu ushindi huu, Yerevan inashuku Azerbajani kuwa na nia nyingine ya kunyakuwa maeneo mengine dhidi ya Armenia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.