Pata taarifa kuu

Azerbaijan yamshikilia rais wa zamani wa jamhuri iliyojitangaza kujitenga ya Nagorno-Karabakh

Azerbaijan imetangaza kumkamata rais wa zamani wa jamhuri inayotaka kujitenga ya Nagorno-Karabakh. Araïk Haroutiounian, ambaye aliongoza kundi la watu wanaotaka kujitenga hadi mapema mwezi Septemba 2023, amewekwa kizuizini. Anashukiwa "kuongoza vita" na "kukodisha mamluki", "kukiuka kanuni za kimataifa za kibinadamu", ilisema Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Azerbaijan.

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev amekataa kushiriki katika mkutano wa kilele huko Grenada.
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev amekataa kushiriki katika mkutano wa kilele huko Grenada. © REUTERS - ANNEGRET HILSE
Matangazo ya kibiashara

Siku moja kabla, Yerevan ililaani kukamatwa kwa viongozi wa zamani au maafisa wa Nagorno-Karabakh, ikitoa mfano wa kesi ya Araïk Haroutiounian bila kutaja ni lini alikamatwa. Lakini Azerbajan ilikuwa bado haijathibitisha habari hii.

Armenia inashutumu watu kukamatwa "kinyume cha sheria" na "kiholela" na Baku kati ya safu ya viongozi wa zamani wa Nagorno-Karabakh. Mamlaka ya Yerevan imeelezea masikitiko yake kwamba "vikosi vya usalama vya Azerbaijan vinaendelea kukamata watu kiholela", licha ya ahadi za "kuheshimu haki za Waarmenia" huko Nagorno-Karabakh.

Afisa mwingine mkuu wa zamani wa Nagorno-Karabakh, Rouben Vardanian, aliwekwa kizuizini mwishoni mwa mwezi wa Septemba.

Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilitaka haki zake ziheshimiwe, huku watoto wake wakisema "wanahofia usalama na hali ya afya yake ikizidi kudorora". Walibaini kuwa hawana taarifa kuhusu mazingira ya kuzuiliwa kwa baba yao.

Aliyev hashiriki mkutano wa kilele wa Granada

Wiki mbili baada ya mashambulizi makubwa ya vikosi vya Azerbajan ambayo yaliwalazimu karibu wakazi wote wa Armenia kutoroka jamhuri iliyojitangaza kujitawala ya Nagorno-Karabakh, rais wa Azerbajan Ilham Aliev alitarajiwa kushiriki mkutano wa kilele nchini Uhispania, uliotarajiwa kupunguza mvutano wa kikanda.

Lakini katika usiku wa mkutano huu, akiwa amekasirishwa na misimamo ya nchi za Ulaya za kuunga mkono Armenia, Ilham Aliev alifahamisha kuwa hatashiriki mkutano huo. Akilaani "misimamo ya kupinga Azerbaijan", hakuona "muhimu" kushiriki katika mazungumzo katika muundo huu, afisa wa Azerbaijan ameliambia shiriika la habari la AFP.

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian, ambaye atakuwepo Granada, ameelezea kusikitishwa kwake na uamuzi huo wa rais aw Azerbaijan.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.