Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu laki moja watoroka eneo la Nagorno-Karabakh

Idadi ya Waarmenia waliotoroka katika eneo la Nagorno-Karabakh imezidi 100,000 kulingana na Nazeli Baghdassarian, msemaji wa Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian.

Magari yanayobeba wakimbizi kutoka Nagorno-Karabakh yakiwa kwenye foleni kwenye barabara inayoelekea mpaka wa Armenia, Septemba 25, 2023.
Magari yanayobeba wakimbizi kutoka Nagorno-Karabakh yakiwa kwenye foleni kwenye barabara inayoelekea mpaka wa Armenia, Septemba 25, 2023. © David Ghahramanyan / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu rasmi, karibu Waarmenia 120,000 waliishi katika eneo hilo kabla ya tangazo la kufutwa mapema wiki kwa jamhuri hii iliyojitangaza kujitenga.

Zaidi ya watu 100,000 wameondoka katika eneo la Nagorno-Karabakh, kulingana na Nazeli Baghdassarian, msemaji wa Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian. Armenia inaishutumu Azerbaijan kwa "safisha safisha la kikabila" huko Nagorno-Karabakh. Kwa upande wake, Baku inakanusha na kudai kuwa wakazi hao wanaondoka wenyewe.

Neno "safisha safisha la kikabila" lilionekana katika miaka ya 1990, wakati wa vita katika Yugoslavia ya zamani. Inarejelea sera ya makusudi inayolenga kuondoa, kutoka kwa maeneo fulani ya kijiografia, watu kutoka kabila fulani au jamii ya kidini, kwa kutumia vurugu au ugaidi. Hii ndiyo maana halisi iliyotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1994. Neno hili limetumika wakati wa kesi zilizokuwa zikisikilizwa mbele ya mahakama za kimataifa.

Lakini "safisha safisha la kikabila" halitambuliwi kama uhalifu kama unavyofikiria. Watu wanaohusika wanaweza, hata hivyo, kushtakiwa na kuhukumiwa kwa mauaji ya halaiki wakati "safisha safisha la kikabila" litakwenda mbali kwa kuharibifu au kuangamiza jamii nzima. Hili lilitokea wakati Radovan Karadzic, kiongozi wa zamani wa Waserbia wa Bosnia, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani mnamo 2019 kwa mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Aliwajibika, miongoni mwa mambo mengine, kwa mauaji ya Waislamu 8,000 huko Srebrenica.

"safisha safisha la kikabila" pia imetajwa katika migogoro mingine, ile ya Darfur nchini Sudan au hata Burma kwa mauaji dhidi ya jamii ya waislamu wachache ya Warohingya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.