Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Nagorno-Karabakh: Watu kadhaa wakimbilia Armenia, mamlaka yataka msaada wa kimataifa

Kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na mamlaka ya Armenia, zaidi ya wakimbizi 42,500 waliwasili Armenia katika siku chache zilizopita, yaani, theluthi moja ya wakazi wa eneo hili linalotaka kujitenga ambao walikimbia eneo hilo na ambalo linakaribia kushikiliwa na vikosi vya Azerbaijan. Wengi wanatarajia misaada ya kimataifa.

Wakazi wanaokimbia Nagorno-Karabakh wakielekea Armenia kupitia ukanda wa Lachin, Septemba 26, 2023.
Wakazi wanaokimbia Nagorno-Karabakh wakielekea Armenia kupitia ukanda wa Lachin, Septemba 26, 2023. AP - Vasily Krestyaninov
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu Septemba 25, 2023, Baku iliahidi kulinda haki za wakaazi wa Armenia wa Nagorno-Karabakh na kuwaachilia wanajeshi watakaoweka chini silaha zao, lakini matamko mengine yanaibua hofu ya kulipizwa kisasi kutoka kwa mamlaka ya Azerbaijan, hasa mamlaka ikidai kutaka kuwatafuta wahusika wa "uhalifu wa kivita" miongoni mwa wanajeshi wanaotaka kujitenga.

Wakaazi wa Nagorno-Karabakh wanaona huenda wakakumbwa na vitimbi vya ubaguzi wa kikabila, na kufanyiwa dhulma, na ndiyo sababu wanaamua kutoroka makaazi yao kuelekea Armenia, anaeleza mwandishi wetu maalum aliyetumwa huko, Daniel Vallot. Barabara pekee inayowezesha kuingia Armenia ni ile ya ukanda maarufu wa Lachin. 

Kwa jumla, inachukua karibu saa 30 kuondoka Nagorno-Karabakh wakati eneo hilo bado linakabiliwa na upungufu wa petroli, anabainisha mwandishi maalum wa France 24 huko Goris, Taline Oundjian. Watu wanaojitolea huleta maji mpakani yakiwa kwenye mikebe ili magari yaweze kufika angalau mji wa karibu zaidi upande wa pili wa mpaka.

Mji huu unaopatikana upande wa pili wa mpaka unaitwa Goris na una wakazi 20,000. Unakabiliwa na kuwasili kwa makumi ya maelfu ya watu walio katika mazingira magumu ya kiafya. Baadhi yao walilazimika kulala kwenye magari yao ingawa tayari kulikuwa na baridi huko Goris na watu wanajitolea wanasema wamezidiwa na idadi kubwa ya wakimbizi na chakula hawana.

Mamlaka, mashirika mbalimbali, waangalizi katika eneo hilo, wote wanaomba msaada, ujumbe wa uchunguzi au hata waandishi wa habari waweze kuingia Nagorno-Karabakh kuripoti juu ya hali hiyo na kuleta bidhaa ambazo wanazohitaji watu waliolazimika kutoroka makaazi yao.

Sasa, lazima tuhifadhi wakimbizi hawa haraka na kuwatafutia masuluhisho ya makazi nchini Armenia. Waziri Mkuu Nikol Pashinian alitangaza kuwa nchi yake imejitayarisha kukaribisha wakimbizi 40,000, lakini kwa idadi hii, kuna hatari idadi hii izidi  kinyume na inavyofiikiri mamlaka ya Armenia.

Msaada wa kiuchumi na kisiasa kutoka nchi za Ulaya

Wakati wa mchana siku ya Jumanne, helikopta pia zilionekana angani. Azerbaijan ilifungua anga yake kwa Urusi ili iweze kuwahamisha mamia ya waliojeruhiwa vibaya kufuatia mlipuko katika kituo cha mafuta na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.