Pata taarifa kuu

Nagorno-Karabakh: Mazungumzo kati ya Armenia na Azerbaijan yafanyika Brussels

Mazungumzo kwa aminajili ya amani ya kudumu yalifanyika Jumamosi (Julai 15) mjini Brussels kati ya Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev. Mazunumzo haya yanalengo la kumaliza mzozo uliodumu kwa takriban miaka 40 huko Nagorno-Karabakh, eneo lenye wakazi wengi wa Armenia nchini Azerbaijan ambalo lilijitenga mapema miaka ya 1990 lakini lilichukuliwa na Waazeri katika Vita vya majira ya baridi mwaka 2020.

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan kabla ya mkutano katika Baraza la Ulaya huko Brussels Mei 14, 2023.
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan kabla ya mkutano katika Baraza la Ulaya huko Brussels Mei 14, 2023. AFP - KENZO TRIBOUILLARD
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya Jumamosi hii hayakuleta maendeleo makubwa, lakini ni sehemu ya shughuli kubwa ya kidiplomasia, anaripoti mwandishi wetu wa Tbilisi, Régis Genté.

Nikol Pashinian na Ilham Aliyev wamekutana sio chini ya mara tatu katika miezi miwili iliyopita, na Brussels inazungumzia juu viongozi hawa kukutana tena baada ya msimu wa joto.

Kulingana na mwanadiplomasia wa Ulaya aliyehusika katika kesi hiyo, viongozi hao wawili wanaelewana na kuongea kwa heshima na wamekaribiana katika masuala mengi.

Walikubaliana juu ya mambo muhimu, hasa kwa kuwa Nikol Pashinian alitangaza mnamo mwezi Mei kwamba nchi yake inatambua Nagorno-Karabakh kama moja ya maeneo ya Azrbaijani.

Pointi kadhaa za mvutano

Jambo kuu la kushikilia ni kuunda utaratibu wa kulinda haki na usalama wa Waarmenia 120,000 wa Karabakh. Lakini, chaguzi sasa zingejadiliwa juu ya hili.

Vile vile inatumika kwa kufunguliwa kwa njia za mawasiliano, zilizotolewa katika makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwezi Novemba 2020. Lazima tuchukue hatua haraka, wanasema huko Brussels, hali inazidi kuwa ngumu katika ardhi ambapo wakazi wa Karabakh wanazidi kuteseka kutokana na kizuizi kilichowekwa na Baku tangu mwezi Desemba mwaka uliyopita.

Majadiliano haya yanafanyika chini ya usimamizi wa Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, kwa hasira kubwa ya Urusi, ambayo iliilifanya mazungumzo ya amani ili kukomesha "vita vya pili vya Karabakh" na kupeleka kikosi cha karibu wanajeshi 2,000 kuingilia kati mwishoni mwa mwaka 2020. Ikikwama nchini Ukraine, Urusi haiwezi tena kutekeleza jukumu lake kama polisi katika Caucasus Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.