Pata taarifa kuu

Nagorno-Karabakh: Putin amjibu Macron kuhusu mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia

Watu 286 waliuawa mwezi Septemba katika mapigano mapya kati ya Urusi na Azerbaijan. Wakati wa mahojiano yake kwxenye kituo cha France 2, Jumatano jioni Oktoba 12, rais w Ufaransa Emmanuel Macron alimnyooshea kidole cha lawama Vladimir Poutine moja kwa moja juu ya mzozo huu uliotawala kati ya Yerevan na Baku kwa sentensi hii: "Urusi iliingilia mzozo huu, ni wazi ilisaidia Azerbaijan kwa ushirikiano na Uturuki na kuja kudhoofisha Armenia".

Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza katika Mkutano wa kilele huko Astana, Kazakhstan, Ijumaa, Oktoba 14, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza katika Mkutano wa kilele huko Astana, Kazakhstan, Ijumaa, Oktoba 14, 2022. AP - Ramil Sitdikov
Matangazo ya kibiashara

Moscow ilichukizwa na kauli hiyo, hadi rais wa Urusi kumjibu moja kwa moja rais wa Ufaransa kutoka mkutano wa kilele wa Astana. Jibu la kwanza lilikuwa tayari limetoka kwa njia ya diplomasia ya Urusi. Katika taarifa yake iliyotangazwa kwa umma jana, Wizara ya Mambo ya Nje ilizichukulia kauli za Emmanuel Macron kuwa ni za uadui na zisizokubalika kabisa. Kulingana na taarifa hii kwa vyombo vya habari, haya yalikuwa "maneno ya kipuuzi ambayo yanathibitisha kwamba Paris haina nia ya kutunza amani ya kudumu katika eneo hilo". Ikimaanisha kwamba Élysée ndiyo inayochochea vurugu, na sio Urusi.

Ikumbukwe kwamba ni nadra sana kwa Vladimir Putin kutoa maoni juu ya taarifa za kila mmoja. Vladimir Putin amemjibu moja kwa moja Emmanuel Macron. “Taarifa hizi zinaonyesha kutoelewa mwenendo wa mgogoro huo, ukosefu wa taarifa za misimamo ya pande mbalimbali. Kwa hali yoyote, maneno haya si sahihi na hayakubaliki. Iwapo fursa itatokea, tutazungumza tena na rais wa Ufaransa,” amesema.

Katika miezi ya hivi karibuni, Umoja wa Ulaya na Marekani zilichukua hatua katika faili hili bila kufanikiwa kukomesha hali ya kutokuwa na utulivu. Mnamo 2020, Vladimir Putin ndiye ambaye alifanikiwa kupatanisha pande mbili na kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita kwenye eneo lenye mzozo la Nagorno-Karabakh. Ijumaa hii, alimwalika tena Waziri Mkuu wa Armenia na Rais wa Azerbaijan kwenye mkutano mpya wa pamoja nchini Urusi. Hakuna tarehe iliyotangazwa.

Diplomasia ya Azerbaijan mara baada ya kauli hizi za rais wa Urusi kwa upande wake imelaani kauli za rais wa Ufaransa Ijumaa hii, Oktoba 14. Katika taarifa yake, amelaani kauli "zisizokubalika na zenye upendeleo" za rais wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.