Pata taarifa kuu

Macron aomba kuanzishwa tena kwa mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumatano jioni alimtaka mwenzake wa Urusi Vladimir Putin "kurejea kwenye meza ya mazungumzo" na kuahidi kuipa Ukraine mifumo ya ulinzi ya angani, katika kukabiliana na mashambulizi mapya makubwa ya Urusi.

Vita nchini Ukraine ilitawala mahojiano ya Emmanuel Macron kwenye kituo cha televiseni cha France2 mnamo Oktoba 12, 2022.
Vita nchini Ukraine ilitawala mahojiano ya Emmanuel Macron kwenye kituo cha televiseni cha France2 mnamo Oktoba 12, 2022. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

"Leo, kwanza, Vladimir Putin lazima amalize vita hivi, aheshimu uadilifu wa ardhi ya Ukraine na arejee kwenye meza ya mazungumzo," alisema Emmanuel Macron kwenye kituo cha televisheni ya France 2, akimshutumurais wa Urusi kufanya "chaguo" la "kuiweka" Ulaya "katika vita" kwa makombora yake ya siku za hivi karibuni na uhamasishaji wa kuimarisha jeshi lake.

Rais wa Ufaransa, licha ya kukosolewa, ikiwa ni pamoja na Ukraine, hajawahi kuvunja mazungumzo na mkuu wa Kremlin tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24. mehakikisha kwamba ataendelea kuzungumza naye β€œwakati wowote inapobidi”.

Rais amesisitiza kwamba hatimaye itakuwa juu ya Waukraine kuamua ni lini masharti ya mazungumzo yatafikiwa na kwamba lengo lililotajwa liko wazi: kurudi kwa "mipaka ya 1991", kabla ya kunyakuliwa kwa Crimea mnamo 2014 na unyakuzi wa majimbo manne iliyonyakuliwa na Urusi mwishoni mwa mwezi wa Septemba.

Msaada mpya wa kijeshi kwa Kyiv

Hadi wakati huo, Ufaransa itaendelea kuisaidia Ukraine kijeshi kwa kuiipa "rada, mifumo na makombora" dhidi ya mashambulizi ya angani na ndege zisizo na rubani za Urusi, Emmanuel Macron amesema, lakini bila kutaja mfumo gani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.