Pata taarifa kuu

Wanne wauawa Nagorno-Karabakh, mazungumzo kati ya Armenia na Azerbaijan yafanyika Washington

Wanajeshi wanne wa Armenia wameuawa Jumatano, Juni 28, kwa risadi zilizofyatuliwa na wanajeshi wa Azerbaijani huko Nagorno-Karabakh, imesema mamlaka ya eneo hili lililojitenga linalozozaniwa na Armenia na Azerbaijan.

Kituo cha ukaguzi nchini Azerbaijan kwenye lango la Ukanda wa Lachin, eneo pekee la ardhini katika jimbo lililojitenga lenye wakaazi wa Armenia la Nagorno-Karabakh na Armenia, kupitia daraja la Mto Hakari, Mei 2, 2023.
Kituo cha ukaguzi nchini Azerbaijan kwenye lango la Ukanda wa Lachin, eneo pekee la ardhini katika jimbo lililojitenga lenye wakaazi wa Armenia la Nagorno-Karabakh na Armenia, kupitia daraja la Mto Hakari, Mei 2, 2023. AFP - TOFIK BABAYEV
Matangazo ya kibiashara

 

"Vikosi vya Wanajeshi wa Azerbaijan vilifyatua risasi dhidi ya ngome za jeshi la Armenia" katika wilaya za Martouni na Martakert usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, kwa kutumia silaha na ndege zisizo na rubani, Wizara ya Ulinzi ya eneo hili lililojitenga imesema katika taarifa yake kwenye Twitter. "Askari wanne waliuawa kutokana na uchokozi huu mpya wa Azerbaijan", kulingana na chanzo hicho.

Tangazo hili linakuja wakati Washington ikiwa mwenyeji tangu Jumanne wa mazungumzo mapya kati ya Armenia na Azerbaijan yenye lengo la kutafuta suluhu la mzozo wa Nagorno-Karabakh.

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken alikutana siku ya Jumanne na wenzake wa Armenia na Azerbaijan, Ararat Mirzoïan na Djeyhoun Baïramov mmoja baada ya mwingine kabla ya kuwaleta pamoja. Majadiliano hayo yanafanyika kwa faragha na yanatarajiwa kudumu hadi siku ya Alhamisi.

"Tunaendelea kubaini kwamba amani inaweza kufikiwa na kwamba mazungumzo ya moja kwa moja ndio ufunguo wa kutatua masuala ambayo hayajakamilika na kuhitimisha amani ya kudumu na yenye heshima" kwa pande zote mbili, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Maekani, Matthew Miller, siku ya Jumatatu.

Marekani iliwaleta pamoja mawaziri hao wawili mjini Washington mapema mwezi Mei. Majadiliano pia yalifanyika katika wiki za hivi karibuni huko Brussels na Moscow.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.