Pata taarifa kuu

Mapigano makali yatokea kwenye mpaka kati ya Armenia na Azerbaijan

Armenia, imesema wanajeshi wake 50 wameuawa katika makabiliano makali na Azerbaijan, yakiwa ni makabiliano mabaya kati nchi hizo mbili ndani ya miaka miwili.

Mwanajeshi wa Armenia aliyesimama karibu na bendera ya Nagorno-Karabakh mnamo Novemba 25, 2020.
Mwanajeshi wa Armenia aliyesimama karibu na bendera ya Nagorno-Karabakh mnamo Novemba 25, 2020. AP - Sergei Grits
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Armenia, Nikol Pashinyan, amethibitisha kuuawa kwa wanajeshi wake, ambao amesema wamepoteza maisha katika mapigano yaliyoendelea usiku wa kuamkia leo. 

Mataifa haya kwa  zaidi ya miaka 30 sasa yameendelea kukabiliana mara kwa mara, huku vita vya hivi punde vikishuhudiwa,  licha ya Urusi kutangaza ilikuwa imefanikiwa kuleta mwafaka kati ya nchi hizo. 

Kiini cha mzozo huu ni umiliki wa jimbo la Nagorno-Karabakh ambalo kwa mujibu wa ramani ya Kimataifa, lipo nchini Azerbaijan lakini wakaazi wake ni kutoka kabila la Warmenia. 

Mbali na mzozo wa kisiasa kuhusu umiliki wa kisiwa hicho, tofauti za kitamaduni na kiimani zikielezwa pia kuwa chanzo cha mzozo unaoshuhudiwa. Armenia ni nchi ya Kikiristo, lakini Azerbaijan ni nchi ya Kiislamu. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.