Pata taarifa kuu

Armenia na Azerbaijan zazindua maandalizi ya mazungumzo ya amani

Armenia na Azerbaijan zimeamua kuzindua matayarisho ya mazungumzo ya amani kati ya nchi hizi mbili ambazo zilipambana mnamo 2020 kwa udhibiti wa eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh, wizara ya Mambo ya Nje ya Armenia imesema Alhamisi hii katika taarifa.

Wanajeshi wa Armenia wakiwa katika ulinzi kwenye kituo cha ukaguzi cha mpaka na Azerbaijan karibu na kijiji cha Sotk huko Armenia, Juni 18, 2021.
Wanajeshi wa Armenia wakiwa katika ulinzi kwenye kituo cha ukaguzi cha mpaka na Azerbaijan karibu na kijiji cha Sotk huko Armenia, Juni 18, 2021. AFP - KAREN MINASYAN
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Vovayi Pashinyan na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev waliwaagiza mawaziri wao wa mambo ya nje "kuanza maandalizi ya mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili" wakati wa mkutano huko Brussels siku ya Jumatano chini ya upatanishi wa Umoja wa Ulaya, imesema taarifa.

Tume ya nchi mbili ya kufafanua upya mipaka

“Makubaliano yamefikiwa wakati wa mkutano huu (...) kuunda tume ya nchi mbili kuhusu masuala ya kuweka mipaka,” taarifa imeongeza. Tume hii itawajibika hasa kuhakikisha usalama na utulivu kwenye mpaka, kulingana na chanzo hicho. Mkutano wa Brussels ulikuja baada ya mvutano kuibuka tena huko Nagorny-Karabakh, ambapo vikosi vya kulinda amani vya Urusi vimetumwa tangu Novemba 2020.

Armenia yapata hasara kubwa huko Nagorno-Karabakh

Mnamo Novemba 2020, usitishaji mapigano uliotiwa saini chini ya upatanishi wa Urusi kati ya Armenia na Azerbaijan ulimaliza vita vya wiki sita kati ya jamhuri hizi mbili za zamani za Soviet huko Caucasus ambazo zinapigania udhibiti wa eneo hilo la Nagorno-Karabakh. Mgogoro huu, ambao uliua zaidi ya watu 6,500, uliishia kwa kushindwa vibaya kwa Armenia, ambayo ililazimika kusalimisha maeneo makubwa iliyokuwa imedhibiti tangu vita vya kwanza vya ushindi mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Eneo la Nagorny-Karabakh lenye idadi kubwa ya Waarmenia, linaloungwa mkono na Yerevan, ulijitenga kutoka Azerbaijan wakati wa kuanguka kwa USSR (Urusi ya zamani), na kusababisha vita vya kwanza katika miaka ya 1990 ambavyo vilisababisha vifo vya watu 30,000 na kufanya mamia ya maelfu ya watu kuyatoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.