Pata taarifa kuu
UTURUKI-USHIRIKIANO

Uturuki: Ankara yateua mjumbe wake kwa Armenia

Baada ya miongo kadhaa ya uhasama wa pande zote, Uturuki na Armenia wanafikiria kurekebisha uhusiano wao. Wiki hii Ankara ilimteua mjumbe wake kwa Armenia, wakati Yerevan ilibaini kuwa itafanya uteuzi wa "mwakilishi maalum wa mazungumzo" na Uturuki katka siku zijazo.

Mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa mzozo nchini Azerbaijan, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezungumza juu ya uwezekano wa kufunguliwa tena kwa mpaka na Armenia.
Mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa mzozo nchini Azerbaijan, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezungumza juu ya uwezekano wa kufunguliwa tena kwa mpaka na Armenia. Adem ALTAN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili hazijawahi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, na mpaka wao umefungwa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Kwa mtazamo wa Ankara, ushindi wa Azerbaijani huko Nagorno-Karabakh katika msimu wa joto wa mwaka 2020 uliondoa kikwazo kikubwa cha maelewano na Armenia. Ikiwa mpaka wa Uturuki na Armenia umefungwa tangu 1993, ni kwa sababu Uturuki ilikuwa imeonyesha kwa uamuzi huu msaada wake kwa Azerbaijan ambayo ilikuwa imepoteza, wakati huo, vita vya kwanza katika eneo hilo kwa faida ya 'Armenia. Tangu wakati huo, Baku imekuwa ikishinikiza kutofaulu kwa ukaribu wowote, pamoja na makubaliano ya kwanza ya kuhalalisha yaliyofikiwa mnamo mwaka 2009.

Kipaumbele kwa mazungumzo

Lakini tangu Azerbaijan - kwa msaada wa Uturuki, kurejesha udhibiti katika maeneo yaliyokuwa yakizozaniwa mwaka jana, hali imebadilika. Mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa mzozo huo, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alizungumza juu ya uwezekano wa kufunguliwa tena kwa mpaka na Armenia. Majirani hao wawili bado hawajafikia hatua hiyo - kwa sasa suala kumbwa ni kuanza mazungumzo ya moja kwa moja kupitia wajumbe. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki pia ametangaza kufunguliwa kwa safari za ndege za kukodi kati ya Istanbul na mji mkuu wa Armenia, Yerevan.

Armenia inasema iko tayari kurekebisha uhusiano "bila masharti". Inamaanisha: bila kudai katika hatua hii kutambuliwa na Uturuki kwa mauaji ya kimbari ya Waarmenia yaliyotekelezwa na utawala wa kifalme wa Ottoman.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.