Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Azerbaijan yadai kuwatimuwa wanajeshi la Armenia Nagorno-Karabakh

Baku imesema kuwa imechukua udhibiti Jumatano hii Agosti 3 ya ngome kadhaa na kuharibu ngome kadhaa za Armenia huko Nagorno-Karabakh, wakati wa mapigano ambayo yamesababisha vifo vya wanajeshi watatu na kuzua hatari ya vita katika eneo hili la milima.

Wanajeshi wa Armenia wakiwa katika kituo cha ukaguzi huko Nagorno-Karabakh, Novemba 25, 2020.
Wanajeshi wa Armenia wakiwa katika kituo cha ukaguzi huko Nagorno-Karabakh, Novemba 25, 2020. AFP - KAREN MINASYAN
Matangazo ya kibiashara

"Udhibiti umeanzishwa kwenye maeneo muhimu ya milima," ikiwa ni pamoja na vijiji kadhaa, Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan ilisema katika taarifa Jumatano wiki hii, na kuongeza kuwa vikosi vyake viko katika mchakato wa kuimarisha udhibiti kwenye ngome hizi.

Mapema Jumatano hii, Agosti 3, pande zote mbili ziliripoti vifo vya angalau wapiganaji wawili wa Armenia na askari mmoja wa Azerbaijan katika mapigano karibu na Karabakh, na kuzua hatari ya vita vipya baada ya vile vya mwaka wa 2020 katika eneo hili linalozozaniwa kati ya Azerbaijan na Armenia. Matukio haya pia yanahatarisha mazungumzo ya amani ambayo yamekuwa yakifanyika kwa miezi kadhaa kati ya nchi hizo mbili kwa upatanishi wa Umoja wa Ulaya.

Siku ya Jumatano, Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan ilitangaza kifo cha askari mmoja baada ya "mapigano mkali" yalio kuwa yakilenga eneo la jeshi la Azerbaijan katika wilaya ya Lachin, eneo lisilomilikiwa na upande wowote kati ya mpaka wa Armenia na Nagorno-Karabakh. Azerbaijan ilidai kutekeleza kwa kulipiza kisasi operesheni iliyoitwa "Kisasi", ambapo "ngome kadhaa za mapigano za waasi haramu wa Armenia ziliharibiwa".

Wanajeshi wawili wa upande unaotaka kujitenga wa Armenia waliuawa na 14 kujeruhiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Azerbaijan, mamlaka katika eneo hilo imesema, na kulaani "ukiukaji wa wazi wa usitishaji mapigano".

Armenia yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa

Armenia "inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kukomesha tabia na vitendo vya uchokozi vya Azerbaijan na kuzindua taratibu zinazofaa za kufanya hivyo," Wizara ya Mambo ya Nje ya Armenia imesema katika taarifa yake.

Urusi iliishutumu Azerbaijan kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo hilo siku ya Jumatano, na kuongeza kuwa walinda amani wake waliotumwa katika eneo hilo walikuwa wakitafuta "kutuliza" hali. Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliongeza katika taarifa yake kwamba "makao makuu ya jeshi la kulinda amani la Urusi, pamoja na wawakilishi wa Azerbaijan na Armenia, wanachukua hatua za kuleta utulivu."

Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya ulitoa wito Jumatano "kukomeshwa mara moja kwa uhasama". "Ni muhimu kupunguza mvutano, kuheshimu kikamilifu usitishaji mapigano na kurejea kwenye meza ya mazungumzo kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo," msemaji wa mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell alisema katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.