Pata taarifa kuu

Wakimbizi kutoka Nagorno-Karabakh waingia nchini Armenia

Nairobi – Nchi ya Armenia inasema, zaidi ya wakimbizi 1,000 kutoka katika jimbo la Nagorno-Karabakh katika nchi jirani ya Azerbaijan, wamevuka mpaka na kuingia nchini mwao.

Taarifa ya serikali ya Armenia inasema kufikia Jana usiku, ilikuwa imewapokea watu 1,050 wenye kabila la Armenia kutoka jimbo la Nagorno-Karabakh
Taarifa ya serikali ya Armenia inasema kufikia Jana usiku, ilikuwa imewapokea watu 1,050 wenye kabila la Armenia kutoka jimbo la Nagorno-Karabakh REUTERS - DAVID GHAHRAMANYAN
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya serikali ya Armenia inasema kufikia Jana usiku, ilikuwa imewapokea watu 1,050 wenye kabila la Armenia kutoka jimbo la Nagorno-Karabakh.

Watu hao wa ni wa kabila la Kiarmenia, wanaoishi kwenye jimbo hilo ambalo linatambuliwa Kimataifa kama êneo la nchi ya Azerbaijan, wanatarajiwa kuendelea kukimbilia nchini Armenia.

Wiki iliyopita jeshi la Azerbaijan, lilifanya operesheni dhidi ya kundi lenye silaha katika jimbo hilo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200 kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Siku ya Jumatatu, rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, anatarajiwa kusherehekea ushindi wa jeshi lake katika jimbo hilo, wakati atakapokutana na mshirika wake wa karibu rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Ufaransa na Marekani, zimelaani kuhangaishwa kwa wakaazi wa Nagorno-Karabakh na jeshi Azerbaijan, huku rais Emmanuel Macron akisema Ufaransa inafuatilia kwa karibu kinachotokea na kutaka kuheshimiwa kwa ardhi ya Armenia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.