Pata taarifa kuu

Azerbaijan yatangaza ushindi dhidi ya waasi katika eneo la Nagorno-Karabakh

Nairobi – Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, ametangaza ushindi, baada ya wanajeshi wa nchi yake kufanikiwa kudhibiti jimbo lenye utata la Nagorno-Karabakh baada ya mapigano ya saa 24 dhidi ya waasi wenye asili ya Kiarmenia.

Rais Aliyev, amelisifu jeshi la Azerbaijan, baada ya kuwakabili waasi hao, ambao wameripotiwa kujisalimisha
Rais Aliyev, amelisifu jeshi la Azerbaijan, baada ya kuwakabili waasi hao, ambao wameripotiwa kujisalimisha AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Rais Aliyev, amelisifu jeshi la Azerbaijan, baada ya kuwakabili waasi hao, ambao wameripotiwa kujisalimisha.

Baada ya tangazo hilo, serikali nchini humo inasema inadhibiti kikamilifu jimbo hilo lenye maakazi ya watu 120,000 kutoka kabila la Armenia.

Mapigano hayo yamesabisha vifo vya watu zaidi ya 200 wakiwemo raia 10 kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Jimbo la Nagorno-Karabakh linatambuliwa Kimataifa kuwa, lipo Azerbaijan, lakini wakaazi wake wanaonekana kuegemea katika nchi jirani ya Armenia.

Tangu miaka ya 90 , mapigano ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhidiwa katika jimbo hilo, linalotaka kujitawala na kutengana na Azerbaijan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.