Pata taarifa kuu

Yerevan: Azerbajan yawakamata Waarmenia wanaokimbia kwa kuhofia usalama wao

Azerbaijan imetangza kwamba inamshikilia Davit Manoukian, jenerali wa Armenia kutoka Nagorno-Karabakh. Baada ya Rouben Vardanian, kiongozi wa zamani wa wanaharakati wanaotaka kujitengwa, Davit Manoukian ni mtu wa pili ambaye Baku imetangaza kukamatwa kwake.

Kituo cha msaada kwa wakimbizi kutoka eneo la Nagorno-Karabakh, katika kijiji cha mpakani cha Kornidzor, Armenia, Septemba 29, 2023.
Kituo cha msaada kwa wakimbizi kutoka eneo la Nagorno-Karabakh, katika kijiji cha mpakani cha Kornidzor, Armenia, Septemba 29, 2023. © Irakli Gedenidze / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Armenia inasema kuna watu wengine wakiemo maafisa kadhaaambao wanashikiliwa na Azerbaijan. Yerevan inashutumu "kukamatwa kinyume cha sheria" ndani ya safu za raia wanaoondoka katika eneo hilo. Kwa kuondoka Nagorno-Karabakh, Waarmenia wanapaswa kupitia kwenye vituo vya ukaguzi vya vikosi vya Azerbajan. Na kwenye kituo cha mwisho, wanaume wa umri wa kupigana wanarekodiwa. Baku inasema wapiganaji ambao wameweka chini silaha zao wanaweza kusamehewa. "Lakini wale waliofanya uhalifu wa kivita [...] lazima wakabidhiwe kwetu," kimeeleza chanzo cha serikali ya Azerbaijan siku ya Jumanne Septemba 26.

Wapiganaji wa Armenia wana wasiwasi

Operesheni hizi za ukaguzi, zinazoongozwa na Azerbaijan, zinatia wasiwasi jumuiya ya Waarmenia. Kila familia ilikuwa na mpiganaji mmoja au zaidi ambao sasa wanaogopa kukamatwa. Wanaume wengi ambao walitumikia eneo hili katika vita vya kujitenga wanasema kwamba kabla ya kuondoka, walichoma vitabu, kumbukumbu na picha za familia, lakini pia sare, silaha na nyaraka katika jaribio la kufuta kazi yao ya kijeshi.

Mkazi wa zamani wa eneo hilo ameiambia RFI kwamba vikosi vya Azerbaijan vina orodha ya watu wanaotakiwa kuwakamatwa. Kulingana na mkazi huyo, Baku inatafuta wanaume 400. Lakini Azerbaijan, kwa upande wake, haijatangaza hatua hiyo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.