Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

Raia wa Armenia wana hofu ya kuzuka kwa vita vipya na Azerbaijan

Armenia inaendelea kukabiliwa na wimbi la wakimbizi kutoka Nagorno-Karabakh: kwa mujibu wa takwimu za hivi punde zilizotolewa na Yerevan, zaidi ya wakazi 100,000 sasa wametoroka eneo hilo na kukimbilia upande mwingine wa mpaka.

Wakimbizi wa Armenia wanaokimbia Nagorno-Karabakh katika kijiji cha mpakani cha Kornidzor, Oktoba 1, 2023.
Wakimbizi wa Armenia wanaokimbia Nagorno-Karabakh katika kijiji cha mpakani cha Kornidzor, Oktoba 1, 2023. AFP - DIEGO HERRERA CARCEDO
Matangazo ya kibiashara

Kinachoongezwa kwa mzozo huu mkubwa wa kibinadamu ni hofu ya kuzuka kwa mzozo mpya na Azerbaijan. Kwa sababu raia wa Armenia wamechoshwa na hali hiyo: Baku itaanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi ili kudhibiti maeneo yaliyo Kusini-Mashariki mwa nchi.

Katika mstari wa kwanza

Kabla ya vita vya mwaka 2020, ambavyo Armenia ilipoteza, kijiji cha Taegh kililindwa na barafu ya maeneo yaliyodhibitiwa hapo awali na Waarmenia, ambao waliyateka katika miaka ya 1990. Ghafla, kijiji hiki kilijikuta kwenye mstari wa kwanza wa vita. Na, mwezi Aprili mwaka huu, mapigano yalizuka kati ya askari wa Azerbaijan na walinzi wa mpaka wa Armenia.

"Wanajeshi wa Warusi waliondoka waliokuwa wameingilia kati kukomesha uhasama wa pande hizo mbili waliondoka bila kumwonya chifu wa kijiji," anasema Norvard Grigorian, akiwa ameketi juu ya jiwe lililokuwa mbele ya nyumba yake. Na kisha wanajrshi wa Azerbaijan walisonga mbele na askari wetu wakawazuia. Makabiliano hayo yalidumu saa tano au sita, kulikuwa na urushianaji risasi kutoka pande zote. Tangu siku hiyo, tunajua kwamba wanaweza kushambulia wakati wowote ... mara tu ninaposikia kelele, nadhani ni wao. Inatisha kwa kweli. "

Ugaidi ni neno ambalo huja midomoni mwa wakaazi wa vijiji vya mpakani. “Askari wanaweza kuja usiku mmoja, kuingia katika nyumba zetu, kutuua, kutukamata,” anasema Larissa Avagyan. Katika Nagorno-Karabakh, wakati wa vita, kulikuwa na uhalifu mwingi: waliwakata vichwa askari, waliwabaka wanawake. Kwa kweli, wana uwezo wa ukatili wowote. Sio tu kwamba hawaadhibu wahusika wa uhalifu huo, lakini wanatunukiwa zawadi wanaporudi nchini. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.