Pata taarifa kuu

Armenia yaonekana kuikasirisha Urusi kwa kutaka kujiunga na ICC

Wabunge nchini Armenia siku ya Jumanne, Oktoba 3, wameidhinisha hatua muhimu katika harakati za kutaka kujiunga na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC.

Bunge la Armenia liliidhinisha Mkataba wa Roma. Uamuzi huu uliungwa mkono na wabunge 60.
Bunge la Armenia liliidhinisha Mkataba wa Roma. Uamuzi huu uliungwa mkono na wabunge 60. AP - Hayk Baghdasaryan
Matangazo ya kibiashara

Ni hatua ambayo inatarajiwa kuendeleza wasiwasi na mwandani wake Moscow, baada ya Urusi kuionya Armenia dhidi ya kuunga mkono mkataba wa uanzilishi wa ICC.

Zoezi hili la upigaji kura likipeperushwa moja kwa moja mtandaoni, lilionyesha wabunge 60 wakiunga mkono pendekezo hilo huku wabunge 22 wakipinga.

Kura hii ya Armenia imeshiria kuongezeka kwa uhasama kati ya Moscow na Yerevan, ambayo imeikasirikia Kremlin kutokana na dhana ya kutochukua hatua kuhusu malumbano ya muda mrefu kati ya Armenia na Azerbaijani.

Mwezi Septemba, vikosi vya Azerbaijan vilivamia eneo lililojitenga la Nagorno-Karabakh,  na kupata kujisalimisha kwa vikosi vya kujitenga vya Armenia ambavyo vilikuwa vimedhibiti eneo hilo la milima kwa miongo kadhaa.

Urusi ilitoa onyo hilo baada ya mahakama ya ICC mnamo mwezi Machi, kutoa kibali cha kukamatwa kwa Rais Vladimir Putin kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine na usafirishaji haramu wa watoto hadi nchini Urusi, ambapo wanachama wa ICC wangemkamata Putin ikiwa angetembelea nchi husika.

Utawala wa Kremlin ulikuwa umesema kuwa uamuzi wa Armenia wa kujiunga na mahakama hiyo yenye makao yake The Hague nchini Uholanzi, itauchukulia kama uhasama mkubwa.

Armenia yajitetea

Wiki iliyopita, waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, alisema mchakato wa nchi yake kujiunga na ICC na ni haki yao kutekeleza uamuzi huo.

Naye muwakilishi wa masuala ya sheria ya kimataifa, Eghishe Kirakosyan, aliliambia bunge kuwa uamuzi huo unalenga wasiwasi wa usalama wa nchi hiyo

Nchi ya Armenia ilitia saini Mkataba wa Roma mwaka 1999, lakini haikuidhinisha, ikisema ikifanya hivyo itakuwa inaenda kinyume cha katiba, lakini mwezi Machi mahakama ya kikatiba ilisema vikwazo hivyo vimeondolewa baada ya armenia kuidhinisha katiba mpya mwaka 2015.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.