Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Antony Blinken atua Vietnam, ili kuimarisha uhusiano dhidi ya China

Marekani na Vietnam zilionyesha Jumamosi hii, Aprili 15 nia ya pamoja ya kuimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia katika muktadha wa mivutano mikali ya kikanda. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye yuko mjini Hanoi kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G7 huko Japani, alikutana jana na viongozi wa Vietnam kujadili "ushirikiano wa kimkakati".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto, akikutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, Nguyen Phu Trong chini ya sanamu kubwa la hayati kiongozi wa mapinduzi ya Vietnam Ho Chi Minh katika Makao Makuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam huko Hanoi, Vietnam, Jumamosi, Aprili 15, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto, akikutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, Nguyen Phu Trong chini ya sanamu kubwa la hayati kiongozi wa mapinduzi ya Vietnam Ho Chi Minh katika Makao Makuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam huko Hanoi, Vietnam, Jumamosi, Aprili 15, 2023. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Lengo ni rahisi: ni kwa Marekani kufanya kila linalowezekana kukabiliana na kujiimarisha kwa China katika kanda ya Indo-Pasifiki. Kwa hili, Washington inapaswa kunda muungano wenye uwezo wa kuzuia matarajio ya Beijing dhidi ya Taiwan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, alitangaza kuimarisha kikosi cha kijeshi nje ya Vietnam: "Kama sehemu ya ushirikiano wetu wa usalama wa nchi mbili, unaoendelea, amesema, tunakamilisha uhamisho wa 'uzinduzi wa tatu wa Walinzi wa Pwani wa Marekani nchini Vietnam, inayosaidia kundi la boti 24 za doria na vifaa vingine, vifaa vya mafunzo na uendeshaji ambavyo tumetoa tangu 2016. Juhudi hizi zote zinaimarisha uwezo wa Vietnam wa kuchangia amani na utulivu wa baharini katika Bahari ya Kusini ya China. "

Nchi nyingi katika kanda hiyo zinasitasita kumpinga jirani wao mkubwa, ambaye sio tu kwamba ni yenye nguvu kijeshi, bali pia mshirika mkuu wa kibiashara na chanzo cha uwekezaji. Licha ya hofu inayohusishwa na mazoezi ya China katika eneo hilo, kuimarisha uhusiano na Marekani bila kuivuruga Beijing ni zoezi nyeti kwa Hanoi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.