Pata taarifa kuu

Luteka kubwa ya kijeshi kati ya Ufilipino na Marekani yaanza Jumanne hii

Ufilipino na Marekani zimeanza mazoezi yao makubwa ya kijeshi ya pamoja ambayo hayajawahi kufanyika katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia, huku washirika wa muda mrefu wakijaribu kukabiliana na ushawishi unaoongezeka wa China katika eneo hilo.

Mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Ufilipino katika kambi ya Fort Magsaysay, karibu na Manila.
Mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Ufilipino katika kambi ya Fort Magsaysay, karibu na Manila. © Romeo Ranoco / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi 18,000 wa Marekani na Ufilipino watashiriki katika mazoezi hayo yatakayochukua muda wa wiki mbili. Mazoezi hayo yatajumuisha kwa mara ya kwanza zoezi la urushaji risasi za moto katika Bahari ya kusini mwa China, ambayo Beijing inadai kuwa ni milki yake. Mojawapo ya mazoezi hayo yatashirikisha kutua kwa helikopta za kijeshi kwenye kisiwa cha Ufilipino kwenye pwani ya kaskazini mwa kisiwa kikuu cha Luzon, karibu kilomita 300 kutoka Taiwan.

'Ushirikiano wa bega kwa bega'

Uzinduzi wa mazoezi haya ya kila mwaka ya Balikatan, neno linalomaanisha "bega kwa bega" kwa Kifilipino, unakuja baada ya operesheni ya kijeshi ya siku tatu iliyohitimishwa Jumatatu Aprili 10 na Beijing, ambayo yalijumuisha mashambulizi na kuzunguka kisiwa kinachojitawala cha Taiwan, ambacho China inachukulia kuwa sehemu ya ardhi yake. Hata hivyo, meli za kivita za China na ndege bado ziko karibu na Taiwan leo Jumaini Aprili 11, Taipei imeripoti. Ukaribu na Taiwan unaweza kuifanya Ufilipino kuwa mshirika mkuu wa Marekani katika tukio la uvamizi wa China dhidi ya kisiwa cha cha Taiwan ambacho inakiona kuwa sehemu yaardhi yake.

Kwa mara ya kwanza, mazoezi haya ya kila mwaka yanafanyika chini ya mamlaka ya Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr, ambaye anatafuta kuboresha uhusiano na Washington, ulioharibiwa na mtangulizi wake Rodrigo Duterte. "Kupitia zoezi hili, vikosi vya Ufilipino na Marekani vitaimarisha ushirikiano wetu, kuongeza ujuzi wetu na kukamilisha uwezo wetu kupitia ushirikiano, ambao utatuwezesha kuwa tayari kukabiliana na changamoto za ulimwengu pamoja", amesema jenerali wa kikosi cha 1 cha wanaanga cha Marekani, U.S. Marine Air. Kitengo (1st MAW) Eric Austin wakati wa hafla ya ufunguzi Jumanne huko Manila.

Katika miezi ya hivi karibuni, Manila na Washington zimezindua upya doria zao za pamoja za baharini katika Bahari ya Kusini ya China, na kufikia makubaliano yenye lengo la kuongeza uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Ufilipino. Chini ya makubaliano hayo, wanajeshi wa Marekani wataruhusiwa kutumia kambi nne mpya za kijeshi za Ufilipino, ikiwa ni pamoja na kambi ya wanamaji isiyo mbali na Taiwan.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.