Pata taarifa kuu

Jeshi la China lazindua mazoezi ya 'kuizingira' Taiwan

Jeshi la China limezindua Jumamosi hii, Aprili 8, siku tatu za mazoezi makubwa ya kijeshi huko Taiwan, katikati ya mvutano na kisiwa hicho baada ya mkutano wa Rais Taiwan Tsai Ing-Wen na Kevin McCarthy, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani nchini Marekani. Kevin McCarthy ni kionngozi mkuu wa tatu nchini Marekani. Manoari nane za kivita na ndege 42 za kivita zimenaswa karibu na kisiwa hicho na Wizara ya Ulinzi ya Taiwan Jumamosi hii, Aprili 8.

Katika picha hii iliyochapishwa na shirika la habari la Xinhua, ndege za kivita za Jeshi la Watu wa Ukombozi wa China (APL) hufanya mafunzo ya pamoja karibu na kisiwa cha Taiwan.
Katika picha hii iliyochapishwa na shirika la habari la Xinhua, ndege za kivita za Jeshi la Watu wa Ukombozi wa China (APL) hufanya mafunzo ya pamoja karibu na kisiwa cha Taiwan. AP - Gong Yulong
Matangazo ya kibiashara

Luteka hii ya siku tatu iliyoandaliwa na Beijing 'hutumika kama onyo kubwa dhidi ya ujumuishaji kati ya vikosi vya kujitenga vinavyotafuta" uhuru wa Taiwan "na vikosi vya nje, na vile vile shughuli zao za uchochezi," amesema msemaji wa Jeshi la China, Shi Yi, katika taarifa. 

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya China, itakuwa mazoezi ya 'kuizingira' Taiwan. Ndege 42 na manoari 8, zimenaswa siku ya kwanza ya mazoezi ya kijeshi ya Beijing kwenye lango la Taiwan. Ndege ishirini na tisa zimezidi mstari unatenganisha China na Taiwan, imesema wizara hiyo, ikilaani "vitendo visivyo vya kawaida". "Katika miaka ya hivi karibuni, tumekuwa tukikabiliwa na upanuzi unaoendelea wa kiimla," amesema Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen, na kuongeza kuwa kisiwa hicho "kitaendelea kufanya kazi na Marekani na nchi zingine (...) kutetea maadili hayo ya uhuru na demokrasia ”.

Mbali na kupelekwa kwa vitengo mbalimbali vya jeshi, mazoezi halisi yakwa kutumia silaha za kivita yatafanyika Jumatatu katika eneo la Taiwan karibu na mipaka ya Fujian (Mashariki), mkoa unaokabili kisiwa hicho, viongozi wa baharini wa eneo hilo wamesema. Kwa kuujibu, Taipei aimesema mazoezi haya yanatishia "utulivu na usalama" katika mkoa wa Asia-Pacific.

Matangazo haya yanafuata ziara ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen nchini Marekani wiki hii, ambapo alikutana Jumatano Aprili 5 na Kevin McCarthy, Spika wa Baraza la Wawakilishi. Wakati huo, Beijing iliahidi kulipiza kisasi kwa "hatua thabiti na zenye nguvu". Kwa sababu China imeona kutoridhika na kazi hiyo katika miaka ya hivi karibuni kati ya mamlaka ya Taiwan na Marekani, ambayo licha ya kukosekana kwa uhusiano rasmi hukipa kisiwa hicho msaada mkubwa wa kijeshi.

China inachukulia Taiwan (yenye wakaazi milioni 23) kama moja ya majimbo yake, ambayo bado hayajaweza kuleta pamoja na eneo lake lote tangu kumalizika kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China mnamo 1949. Marekani ilitambua Jamhuri ya Watu wa China Mnamo 1979 na kwa nadharia haipaswi kuwa na mawasiliano yoyote rasmi na Jamhuri ya China (Taiwan), chini ya "kanuni ya China moja" Beijing imebaini.

Shinikizo la kijeshi

Tangu Aprili 6, Beijing imeongeza shinikizo la kijeshi kwa Taiwan na kupelekwa kwa meli za kivita na ndege kwenda kwenye lango la Taiwan. 

Mnamo Agosti, Beijing ilizindua luteka ya kijeshi ambayo haijawahi kufanywa karibu na Taiwan wakati Nancy Pelosi, ambaye alitangulia Bwana McCarthy kwenye nafasi ya spika wa Baraza la Wawakilioshi la Marekani, alizuru kisiwa hicho. 

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.