Pata taarifa kuu

Marekani: Mahakama ya Rufaa yakataa ombi la Trump la kinga ya uhalifu

Mahakama ya Rufaa ya Marekani siku ya Jumanne imefutilia mbali ombi la Donald Trump la kinga ya uhalifu, na kufungua tena njia ya kusikilizwa kwake huko Washington kwa tuhuma za kujaribu kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 kinyume cha sheria.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, katika mahakama ya New York, kwa ajili ya ufunguzi wa kesi yake, Oktoba 2, 2023.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, katika mahakama ya New York, kwa ajili ya ufunguzi wa kesi yake, Oktoba 2, 2023. © Brendan McDermid / AP
Matangazo ya kibiashara

 

"Tumejaribu kuchunguza madai ya rais wa zamani Trump kuhusu kinga dhidi ya masilahi muhimu ya umma katika kuruhusu utaratibu huu kuendelea," wanaeleza majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa katika uamuzi wao wa kuthibitisha hilo lililotamkwa mara ya kwanza mnamo mwezi wa Desemba.

"Kwa madhumuni ya kesi hii ya jinai, rais wa zamani Trump amekuwa raia kama wengine, kwa sasa ni raia Trump, na ana ulinzi sawa na mshtakiwa mwingine yeyote. Lakini kinga yoyote inayotolewa kwa viongozi, ambayo ingeweza kumlinda alipokuwa rais madarakani, haimlindi tena dhidi ya mashtaka haya,” wanaandika.

Hata hivyo uamuzi huo haujumuishi kutajwa kwa shauri la kurejeshwa kwa taratibu za kisheria katika kesi hii, zilizositishwa kutokana na rufaa hiyo na kupelekea jaji atakayesimamia mjadala kwa kesi hiyo,  iliyopangwa kusikilizwa Machi 4 kutangaza siku ya Ijumaa kuahirishwa kwa muda usiojulikana.

Jaji Tanya Chutkan amebaini kwamba "mahakama ingeamua tarehe mpya" ikiwa, mara tu suala la kinga litaamuliwa, faili hiyo itarudi mikononi mwake. Ni yeye ambaye alikataa ombi lake la kinga mnamo mwezi wa Desemba, kwa kuzingatia kwamba hakuna maandishi yaliyomlinda rais wa zamani dhidi ya mashtaka ya jinai.

Trump atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo

Kiongozi anayepewa nafasi zaidi ya kushinda katika kura za mchujo za chama cha Republican, kwa uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba, anaomba kupitia rufaa nyingi ili kuahirisha kesi zake mbalimbali za uhalifu, angalau hadi baada ya uchaguzi. Donald Trump atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa Mahakama ya Rufaa, msemaji wake Steven Cheung ameliambia shirika la habari la AFP.

Wakati wa mijadala mbele ya Mahakama ya Rufaa mnamo Januari 9 juu ya rufaa yake ya kinga, alitabiri "kutakuwa na machafuko nchini" ikiwa vyombo vya sheria vya Marekani havitafuta kesi dhidi yake.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.