Pata taarifa kuu

Antony Blinken azuru Mexico kujaribu kutatua suala gumu la wahamiaji wanaoelekea Marekani

Kutokana na wimbi jipya la wahamiaji katika mpaka wa kusini mwa Marekani, mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken anasafiri kuelekea Mexico siku ya Jumatano kujaribu kutafuta suluhu na Rais Andres Manuel Lopez Obrador. Siku ya Jumapili, msafara wa maelfu ya wahamiaji uliondoka kusini mwa Mexico kwa kujaribu kuingia nchini Marekani.

Msafara wa wahamiaji nchini Mexico ukielekea Marekani, Desemba 26, 2023.
Msafara wa wahamiaji nchini Mexico ukielekea Marekani, Desemba 26, 2023. © JOSE TORRES / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken anasafiri kuelekea Mexico siku ya Jumatano, Desemba 27, kujaribu kutafuta suluhu la wimbi jipya la wahamiaji mpakani, mada ya mjadala mkali wa kisiasa nchini Marekani.

Ziara hii ya nadra waka wasikukuu za mwisho wa mwaka inakuja wakati ambapo wabunge wa chama cha Republican katika Baraza la Congress wanadai makubaliano juu ya uhamiaji na serikali ya Joe Biden ili kubadilishana na msaada wao kwa kifurushi kipya cha msaada kwa Ukraine.

Vivuko vya mpakani vimefungwa

Katika wiki za hivi karibuni, watu wapatao 10,000 kwa siku wamejaribu kuvuka mpaka wa kusini wa Marekani kinyume cha sheria, karibu mara mbili ya idadi ya kabla ya janga la Uviko- 29. Na msafara wa maelfu ya wahamiaji uliondoka kusini mwa Mexico siku ya Jumapili kujaribu kuelekea Marekani.

Kundi la wahamiaji walioingia Marekani kutoka Mexico katika eneo la Eagle Pass, Texas, wakisikiliza maagizo yanayotolewa na afisa wa Doria ya Mipaka, Agosti 25, 2023.
Kundi la wahamiaji walioingia Marekani kutoka Mexico katika eneo la Eagle Pass, Texas, wakisikiliza maagizo yanayotolewa na afisa wa Doria ya Mipaka, Agosti 25, 2023. AFP - SUZANNE CORDEIRO

Kwa kuzidiwa na wimbi hili la wahamiaji, mamlaka ya Marekani imelazimika kufunga vivuko vya mpaka ili kukabiliana na wahamiaji wanaojaribu kuvuka kinyume cha sheria.

Mexico, baada ya makubaliano na Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump, inawapokea katika ardhi yake wahamiaji wanaotaka kuingia Marekani.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.