Pata taarifa kuu

Mexico: Msafara wa wahamiaji, hasa Wavenezuela, njiani kuelekea Marekani

Msafara mpya wa wahamiaji, hasa wenye asili ya Venezuela, uliondoka wikendi hii kutoka mpaka wa kusini mwa nchi hiyo. Ni aina ya maandamano dhidi ya sera mpya ya Marekani, yenye vikwazo zaidi vya uhamiaji, ambayo inajaribu kudhibiti wimbi la wahamiaji kwenye mpaka wake na Mexico.

Msafara huo mpya wa wahamiaji, hasa wenye asili ya Venezuela, uliondoka wikendi hii kutoka mpaka wa kusini mwa nchi hiyo. Ni aina ya maandamano dhidi ya sera mpya ya Marekani, yenye vikwazo zaidi vya uhamiaji, ambayo inajaribu kudhibiti wimbi la wahamiaji kwenye mpaka wake na Mexico.
Msafara huo mpya wa wahamiaji, hasa wenye asili ya Venezuela, uliondoka wikendi hii kutoka mpaka wa kusini mwa nchi hiyo. Ni aina ya maandamano dhidi ya sera mpya ya Marekani, yenye vikwazo zaidi vya uhamiaji, ambayo inajaribu kudhibiti wimbi la wahamiaji kwenye mpaka wake na Mexico. REUTERS - JOSE LUIS GONZALEZ
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu waliondoka katika jiji la Tapachula katika jimbo la Chiapas kusini mwa Mexico. Wahamiaji hao wengi wakiwa ni raia wa Venezuela, waliondoka kwa miguu kwenye mvua na joto kali wakiwa na matumaini ya kufika Marekani kilomita 2,800 kaskazini. Lakini wakati huo huo, Taasisi ya Uhamiaji ya Mexico imekumbusha kwamba Wavenezuela wote wanaoandamana nchini humo kwa misafara hawataweza kuomba hifadhi nchini Marekani.

Ikiwa watajaribu kuvuka mpaka, watafukuzwa moja kwa moja na hawataweza tena kuanza mchakato mpya wa kuwa wakimbizi. Hili ni mojawapo ya masharti ya makubaliano mapya ya kibinadamu ya serikali ya Marekani. Sasa inawahitaji Wavenezuela wanaotaka kusafiri kwenda Marekani kutuma maombi ya visa wakiwa nje ya nchi.

Ni lazima pia wawe na mdhamini nchini Marekani ambaye anaweza kukidhi mahitaji yao na lazima wafike kwa ndege. Chini ya masharti haya, Marekani itakubali raia 24,000 kutoka Venezuela. Lakini ni tone la maji machoni pa wale wote wanaokimbia utawala wa Nicolas Maduro na mzozo wa kiuchumi. Mwezi Septemba pekee, wakimbizi 33,000 walizuiliwa kwenye mpaka wa Marekani. Tangu mwezi Oktoba 2021, Wavenezuela 155,000 wameingia Marekani kupitia mpaka wa Mexico, idadi ambayo imeongezeka mara tatu katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.