Pata taarifa kuu

Cuba na Marekani zarejelea majadiliano yao kuhusu suala la uhamiaji

Walinzi wa mpaka wa Cuba na Marekani wamekutana kwa siku mbili huko Havana ili kufufua ushirikiano katika vita dhidi ya biashara haramu na uhamiaji haramu.

Baadhi ya Wakazi wanasubiri kuingia katika duka moja katikati mwa Havana mnamo Julai 29, 2022.
Baadhi ya Wakazi wanasubiri kuingia katika duka moja katikati mwa Havana mnamo Julai 29, 2022. © Alexandre Meneghini / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Cuba ndio iliyotangaza mkutano huu wa huduma za walinzi wa mpaka wa nchi hizo mbili, Alhamisi na Ijumaa. Mkutano wa "kiufundi" unaohusu uhamiaji haramu, uokoaji baharini, usafirishaji wa binadamu na dawa za kulevya

Mkutano huo ulifanyika katika hali ya "heshima na kitaaluma" kulingana na Minint, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Cuba.

Cuba inakabiliwa na wimbi la uhamiaji: zaidi ya watu 177,000 waliingia Marekani kupitia mpaka wa Mexico kati ya mwezi wa Oktoba 2021 na mwezi wa Julai 2022, kulingana na mamlaka ya Marekani. Na safari ya baharini inakabiliwa tena na upanuzi mkubwa: balseros 5,421, wahamiaji hawa ambao walipanda boti, na kurudishwa kisiwani wakati huo huo, kulingana na walinzi wa pwani ya Cuba, wengi wakisafiri wakati wa miezi ya majira ya joto.

Hii ni takwimu ya juu zaidi tangu mgogoro mkubwa wa uhamiaji wa 1994 wakati watu 35,000 walihama. Watu wanaoondoka kuelekea Marekaniwanapitia ufuo huu mdogo kilomita 30 kutoka Havana ambao Wacuba wameuita kwa kejeli "Terminal 3". Mgogoro mkubwa wa kiuchumi ambao kisiwa hicho kinapitia na uhaba bidhaa mbalimbali unaoongezeka ni moja ya sababu kubwa za watu kuitoroka nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.