Pata taarifa kuu

Marekani: Idadi ya wahamiaji yazidi kuongezeka kwenye mpaka na Mexico

Wahamiaji wanaendelea kuwasili katika mpaka wa Marekani na Mexico wenye ulinzi mkali, huku polisi ya mpakani ikisimamisha zaidi ya vivuko milioni 1.8 kwenye mpaka wake katika mwaka wa fedha wa 2023. Maelfu ya watu wanaokimbia nchi zao wamewasili katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya mpakani huko Texas.

Wahamiaji wanajaribu kuvuka kwa miguu Mto wa Rio Grande, mpaka wa asili kati ya Marekani na Mexico.
Wahamiaji wanajaribu kuvuka kwa miguu Mto wa Rio Grande, mpaka wa asili kati ya Marekani na Mexico. © Julio Cesar Aguilar - AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Agosti, Marekani ilitangaza kuwa itaanzisha mpango wa msaada kwa wakimbizi. Mwezi uliopita, wahamiaji 232,972 walivuka mpaka wa kusini, idadi iliyoongezeka ikilinganishwa na miezi iliyopita.

Idadi ya wahamiaji barabarani na kaskazini mwa Mexico inafikia rekodi kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji. Tangu majira ya kiangazi, idadi ya watu waliokamatwa na polisi ya mpakani nchini Marekani iliendelea kuongezeka kwa kishindo mwezi Agosti. Idadi ya wakimbizi inaongezeka na shinikizo linaongezeka kwenye mpaka - wiki iliyopita mamlaka ya Marekani iliamua kufunga Eagle Pass, daraja linalounganisha mji wa Piedras Negras katika jimbo la Coahuila na Texas. Wahamiaji wengi hutokea nchini Mexico, lakini pia kupitia, hivyo idadi ya wahamiaji ikiongezeka ndani ya nchi. Katika mpaka wa kusini, inakadiriwa kuwa karibu watu 6,000 huingia nchini Mexico kila siku. Idara ya huduma za hifadhi za Mexico zimezidiwa kabisa. Na barabarani, wahamiaji hufanya kila wawezalo kwenda kaskazini. Kiasi kwamba wiki iliyopita shirika kuu la reli la Mexico lilisimamisha sehemu ya shughuli zake kwa sababu ya maelfu ya watu waliokuwa wakijihatarishia maisha kwa kuingia kwenye magari ya mizigo.

Ufumbuzi wa kijeshi

Kutokana na dharura hii, Marekani inajibu kwa ufumbuzi wa kijeshi. Idara ya Usalama ya Marekani imetangaza kutumwa kwa maafisa 800 wa polisi kwenye mpaka ili kusaidia wanajeshi 2,500 wkutoka kikosi cha walinzi wa taifa ambao wako eneo hilo. Kwa upande wake, Mexico imekubaliana na shirika la reli na mamlaka ya Marekani kuongeza idadi ya wahamiaji wanaorudi katika nchi ya asili na kujaribu kupunguza shinikizo kwenye mpaka. Lakini kinachokosekana ni jibu la kina kwa sababu za msingi za tatizo hilo. Huu pia ni wito uliyozinduliwa siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico kwa Umoja wa Mataifa. Anazitaka nchi kufanya juhudi za kupunguza kukosekana kwa usawa kati ya mipaka na kuzingatia mgogoro huu kama mgogoro wa kibinadamu. Mpaka wa ardhini kati ya Marekani na Mexico ndio hatari zaidi duniani, na wale wanaovuka Río Grande wana hatari ya kuzama. Wiki iliyopita pekee watu wawili walikutwa wamekufa majini, akiwemo mtoto wa miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.