Pata taarifa kuu

Marekani: Mradi wa kizuizi kinachoelea kwenye Rio Grande kuzuia wahamiaji wazua utata

Baada ya kutangazwa na Gavana wa Texas Greg Abbott, kutoka chama cha Republiacan, siku ya Alhamisi, mradi huu unapanga kufunga maboya makubwa yanayoelea kwenye mto ili kuwazuia wahamiaji kujaribu kuvuka.

Mto Rio Grande, ambao asili yake ni Milima ya Rocky huko Colorado (magharibi) kabla ya kuvuka New Mexico na Texas na kutiririka kwenye Ghuba ya Mexico (kusini-mashariki), hufanya kama mpaka wa asili na wa kimataifa kati ya Marekani na Mexico kwa takriban kilomita 2000. Huko Mexico unaitwa Rio Bravo. Pia unatawaliwa na mikataba kati ya nchi hizi mbili.
Mto Rio Grande, ambao asili yake ni Milima ya Rocky huko Colorado (magharibi) kabla ya kuvuka New Mexico na Texas na kutiririka kwenye Ghuba ya Mexico (kusini-mashariki), hufanya kama mpaka wa asili na wa kimataifa kati ya Marekani na Mexico kwa takriban kilomita 2000. Huko Mexico unaitwa Rio Bravo. Pia unatawaliwa na mikataba kati ya nchi hizi mbili. © Julio Cesar Aguilar - AFP
Matangazo ya kibiashara

Kesi iliwasilishwa siku ya Jumamosi dhidi ya mpango wa jimbo la Texas nchini Marekani kupeleka kizuizi kinachoelea kwenye Mto wa Rio Grande ili kuzuia kuvuka kwa wahamiaji haramu kutoka Mexico.

Mradi huu uliowasilishwa Alhamisi na Gavana wa Texas Greg Abbott unapanga kusakinisha maboya makubwa yanayoelea kwenye mto ili kuwazuia wahamiaji hawa, waliopewa jina la utani kwa lugha ya Kihispania "espaldas mojadas" (migongo yenye unyevunyevu) wasijaribu kuvuka.

"Usakinishaji huu unaanza leo," gavana huyo alitangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya Ijumaa, akichapisha picha za lori zilizobeba maboya makubwa yenye rangi ya machungwa.

Yasambazwa kwa karibu mita 300

Mto Rio Grande, ambao asili yake ni Milima ya Rocky huko Colorado (magharibi) kabla ya kuvuka New Mexico na Texas na kutiririka kwenye Ghuba ya Mexico (kusini-mashariki), hufanya kama mpaka wa asili na wa kimataifa kati ya Marekani na Mexico kwa takriban kilomita 2000. Huko Mexico unaitwa Rio Bravo. Pia unatawaliwa na mikataba kati ya nchi hizi mbili.

"Maboya haya yatazuia watu kukaribia mpaka. Na mchakato huu unaanza mara moja", pia alitangaza gavana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

Steve McCraw, mkurugenzi wa idara inayohusika na usalama wa umma, kwa upande wake, alibainisha wakati wa mkutano huu kwamba mfumo huo ulikusudiwa kuwazuia wahamiaji kujaribu kuvuka na kuzama na kwamba ulitumwa kwa takriban mita 300 kwa urefu kutoka sehemu ya kuvuka inayoitwa Eagle Pass.

Mjasiriamali awasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama

Gavana Greg Abbott mara kwa mara anamshutumu Rais wa chama cha Democratic Joe Biden kwa kutochukua hatua zinazohitajika kuzuia kuwasili kwa mawimbi ya wahamiaji kutoka Mexico, na ametangaza kuwa atachukua hatua yeye mwenyewe.

Utawala wa shirikisho la Marekani haukujibu mara moja tangazo hili, lakini mjasiriamali wa ndani alikuwa wa kwanza siku ya Jumamosi kujaribu kuzuia hatua hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.