Pata taarifa kuu

Ajali nchini Mexico: Kumi wafariki na 25 kujeruhiwa kati ya wahamiaji waliokuwa wakisafiri kwa lori

Takriban wahamiaji kumi wamefariki na wengine 25 kujeruhiwa Jumapili Oktoba 1 wakati lori walimokuwa wakisafiria kinyume cha sheria kupinduka kwenye barabara kuu katika jimbo la Chiapas, kusini mwa Mexico, kwenye mpaka na Guatemala, kulingana na mamlaka katika eneo hilo. Ripoti ya muda iliyotumwa na mamlaka inaonyesha "watu kumi wamefariki na 25 kujeruhiwa".

Kundi la wahamiaji walioingia Marekani kutoka Mexico katika eneo la Eagle Pass, Texas, wakisikiliza maagizo yanayotolewa na afisa wa Doria ya mipaka, Agosti 25, 2023.
Kundi la wahamiaji walioingia Marekani kutoka Mexico katika eneo la Eagle Pass, Texas, wakisikiliza maagizo yanayotolewa na afisa wa Doria ya mipaka, Agosti 25, 2023. AFP - SUZANNE CORDEIRO
Matangazo ya kibiashara

Maafa mapya kwenye barabara ya kuelekea Marekani. Takriban wahamiaji kumi walikufa na wengine 25 kujeruhiwa siku ya Jumapili wakati lori walimokuwa wakisafiria kinyume cha sheria lilpinduka kwenye barabara kuu katika jimbo la kusini mwa Mexico la Chiapas kwenye mpaka na Guatemala, kulingana na mamlaka ya eneo hilo.

Ripoti ya muda iliyotumwa na mamlaka inaonyesha "kumi wamekufa na watu 25 kujeruhiwa". Chanzo cha habari kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka ambacho kiliomba kutotajwa jina, kilidokeza kuwa waliofariki ni wanawake akiwemo mtoto mdogo kutoka Cuba.

Ongezeko la wahamiaji kwenye mpaka wa Mexico

Ajali hiyo ilitokea mapema asubuhi kwenye sehemu ya barabara kuu inayounganisha Pijijiapan naTonalá, kwenye pwani ya Pasifiki ya jimbo la Chiapas, ambako wahamiaji wengi wanaotaka kufika Marekani wanatoka. Hii ni ajali ya pili ya aina hii ndani ya wiki moja. Wahamiaji wawili walifarikina na wengine 27 kujeruhiwa siku ya Alhamisi wakati lori lililokuwa limewabeba lilipopinduka katika jimbo hilo.

Maelfu ya wahamiaji wa mataifa tofauti huvuka Mexico kwa mabasi, malori na hata treni za mizigo katika jaribio la kufika Marekani. Doria ya Mipaka ya Marekani ilirekodi rasmi vivuko vya wahamiaji milioni 1.8 katika mpaka wake wa kusini kati ya mwezi Oktoba 2022 na mwezi Agosti 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.