Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-HAKI

Mexico: Mtoto wa 'El Chapo' asafirishwa kwenda Marekani

Mexico imeikabidhi Marekani mtoto wa Joaquin 'El Chapo' Guzman, mamlaka ya Marekani ilitangaza Ijumaa hii, Septemba 15. Alikamatwa mnamo mwezi Januari 2023 wakati wa operesheni iliyogharimu maisha ya askari kumi wa Mexico na wahalifu karibu ishirini. 

Kusafirishwa nchini Marekani kwa Ovidio Guzman Lopez (picha yetu) kunaonyesha wale waliotilia shaka dhamira ya DEA, shirika la Marekani la kupambana dhidi ya dawa za kulevya, katika vita vyake dhidi ya shirika la Sinaloa.
Kusafirishwa nchini Marekani kwa Ovidio Guzman Lopez (picha yetu) kunaonyesha wale waliotilia shaka dhamira ya DEA, shirika la Marekani la kupambana dhidi ya dawa za kulevya, katika vita vyake dhidi ya shirika la Sinaloa. AFP - HO
Matangazo ya kibiashara

Mtoto wa mlanguzi wa dawa za kulevya maarufu zaidi anashutumiwa na Marekani kwa kusimamia maabara zinazozalisha methamphetamine katika jimbo la Sinaloa, iliyokuwa ngome ya zamani ya baba yake ambaye sasa anatumikia kifungo cha maisha jela katika gereza la Marekani.

Uhamisho huu "unaonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali za Marekani na Mexico ili kuzuia ulanguzi wa dawa za kulevya": katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ikitangaza kuhamishwa kwa Ovidio Guzman Lopez, Idara ya Usalama wa Nchi ya Marekani inaelezea sababu kwa nini vyombo vya sheria ilikuwa ikidai: biashara ya dawa za kulevya, utakatishaji fedha, pamoja na uhalifu wa kutumia nguvu.

Operesheni ya umwagaji damu

Mtoto huyu wa "El Chapo" anachukuliwa kuwa kiongozi wa "Menores", kundi linalofanya biashara la Sinaloa ambalo baba yake aliongoza. Kwa jina la utani "El Chapito", aligonga vichwa vya habari wakati wa ziara ya rais wa Marekani nchini Mexico, kwani, siku chache kabla ya kuwasili kwa Joe Biden, ukoo wake ulikabiliana na wanajeshi wa Mexico wakati wa operesheni ya umwagaji damu ambayo ilisababisha vifo vya watu kumi katika safu ya jeshi na wengine kumi na tisa katika kambi ya kundi . Operesheni ambayo, hata hivyo, ilifanya iwezekane kumkamata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.