Pata taarifa kuu

Wamarekani 2 kati ya 4 waliotekwa nyara kaskazini-mashariki mwa Mexico wapatikana wamekufa

Wamarekani wawili kati ya wanne waliotekwa nyara na watu wenye silaha siku ya Ijumaa huko Matamoros, mji ulioko kaskazini-mashariki mwa Mexico kwenye mpaka na Marekani, walipatikana wamefariki siku ya Jumanne, ametangaza gavana wa jimbo la Tamaulipas, Americo Villarreal.

Katibu wa Jeshi la Wanamaji la Mexico Jose Rafael Ojeda wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kutekwa nyara kwa raia wanne wa Marekani, wawili kati yao waliuawa, katika jimbo la Tamaulipas. Ikulu ya Jiji la Mexico, Machi 7, 2023.
Katibu wa Jeshi la Wanamaji la Mexico Jose Rafael Ojeda wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kutekwa nyara kwa raia wanne wa Marekani, wawili kati yao waliuawa, katika jimbo la Tamaulipas. Ikulu ya Jiji la Mexico, Machi 7, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Kati ya hao wanne (Wamarekani), wawili wamekufa, mmoja amejeruhiwa na mwingine yuko hai," gavana amesema kwa simu wakati wa mkutano wa asubuhi wa Rais wa Mexico Andrés Manuel Lopez Obrador na waandishi wa habari.

Wamarekani hao wanne, ambao utambulisho wao bado haujajulikana, walipita katika mji wa Matamoros, katika jimbo la Tamaulipas, wakiendesha gari dogo jeupe lililosajiliwa North Carolina kabla ya kulengwa kwa risasi na kisha kutekwa nyara na watu wenye silaha.

FBI ilitoa zawadi ya dola 50,000 kwa usaidizi wowote utakaochangia kuachiliwa kwao na kukamatwa kwa washukiwa wa Al Shabab.

Mji wa Matomoros umekumbwa na ghasia zinazohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu uliopangwa. Barabara katika eneo hilo zinachukuliwa kuwa hatari zaidi nchini Mexico kutokana na hatari ya utekaji nyara na unyang'anyi wa makundi ya wahalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.