Pata taarifa kuu
USHIRKIANO-DIPLOMASIA

Joe Biden aanza ziara yake rasmi ya kwanza nchini Mexico

Zaidi ya miaka miwili baada ya kuchaguliwa kwake, Rais wa Marekani Joe Biden anaanza ziara yake ya kwanza rasmi nchini Mexico Jumapili hii, Januari 8. Mazungumzo kati ya rais wa Marekani na mwenyeji wake yatajikita katika masuala ya uhamiaji uliokithiri kwenda Marekani, ambapo wahamiaji wengi hupitia wakati mwingi katika nchi hii na utumiaji wa dawa kupita kiasi unaosababishwa na fentanyl, dawa ya syntetisk yenye nguvu zaidi inayozalishwa na makampuni ya Mexico.

Rais wa Marekani Joe Biden (picha yetu) anaanza ziara yake ya kwanza rasmi nchini Mexico Jumapili hii, Januari 8, zaidi ya miaka miwili baada ya kuchaguliwa kwake.
Rais wa Marekani Joe Biden (picha yetu) anaanza ziara yake ya kwanza rasmi nchini Mexico Jumapili hii, Januari 8, zaidi ya miaka miwili baada ya kuchaguliwa kwake. AFP - SAUL LOEB
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden ataanza ziara yake kwa kusimama huko El Paso, mji wa mpakani kusini mwa Texas, njia ya kuwanyamazisha wakosoaji wanaomtuhumu kuwa hajawahi kusafiri zaidi ya kilomita 3,000 za mpaka wa kawaida katika miaka miwili madarakani. Kisha atakuwa katika mji mkuu wa Mexico siku ya Jumatatu Januari 9 kukutana na mwenzake Andres Manuel Lopez Obrador, kabla ya mkutano wa kilele wa pande tatu Jumatano Januari 11 na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Fentanyl

Kabla ya hapo, Joe Biden na Andres Manuel Lopez Obrador watazungumza juu ya uhamiaji, wakati huko Marekani, watu milioni 2.3 walikamatwa na hatua za kufukuzwa kwa wahamiaji wasio na hati zilirekodiwa mwaka jana. Pia kwenye mpango huo ni fentanyl, dawa hii ya syntetisk inayozalishwa na makampuni ya Mexico ambayo inawajibika kwa theluthi mbili ya vifo vya  watu 108,000 katika mwaka 2021 upande wa pili wa Rio Grande.

'Upanuzi wa kupeana taarifa'

Washington inasema inataka 'kupanua ushirikiano wa kupeaa taarifa' na Mexico; nchi ambayo, kabla tu ya ziara hii, ilitangaza, Januari 5, kukamatwa kwa Ovidio Guzman, mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa methamphetamines (na mtoto wa mfanyabiashara wa dawa za kulevya El Chapo Guzman). Hatimaye, mabadiliko ya tabia nchi na juu ya yote ushirikiano katika kile kinachoitwa nishati safi inapaswa pia kushughulikiwa: Mexico inatarajia kunufaika na jitihada za Washington, ambayo inajaribu kupunguza utegemezi wake kwa wazalishaji wa Asia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.