Pata taarifa kuu

Haiti: Mazungumzo yanaendelea UN kwa ajili ya kuunda jeshi la polisi la kimataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halitakutana kuhusu suala la Haiti leo Ijumaa mjini New York. Lakini nchi hizo kumi na tano zitapokea ripoti ya kamati ya wataalam, ambapo wataalam, lakini pia wajumbe wa kamati ya vikwazo na nchi jirani wanawasilisha changamoto zilizoletwa huko Port-au-Prince.

Vikosi vya usalama vikishika doria katika mitaa ya Port-au-Prince, Agosti 5, 2023.
Vikosi vya usalama vikishika doria katika mitaa ya Port-au-Prince, Agosti 5, 2023. © AP/Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Baada ya mwaka wa kusitasita, matumaini ya tahadhari hatimaye yametawala katika Umoja wa Mataifa kuhusu jeshi la polisi la kimataifa la siku zijazo, ambalo linapaswa kusaidia maafisa wa polisi wa Haiti katika mapambano yao dhidi ya magenge yenye silaha, kwa ombi la Port-au- Prince na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa. Azimio la kuundwa kwa kikosi hiki, ambacho kitaidhinishwa lakini hakitasimamiwa na Umoja wa Mataifa, sasa kinajadiliwa kati ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kulingana na habari kutoka RFI, orodha mpya ya watu waliowekewa vikwazo itapendekezwa. Na zaidi ya yote, ripoti itaomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwekeza katika matarajio ya kikosi cha polisi wa kimataifa.

Kenya, ambayo hatimaye ilijitolea kuratibu, ilituma mwezi Agosti watu 30 kwa misheni ya kutathmini nchini Haiti, na ilikubali kutuma maelfu ya maafisa wake wa polisi mashuhuri.

Nchi hii pia imetengeneza orodha ya mahitaji ya vifaa kwa ajili ya kupelekwa kikamilifu kwa maafisa wa polisi. Itabidi sasa kuleta pamoja ufadhili kwa upande mmoja, na maafisa zaidi kwa upande mwingine, angalau 1,000 na zaidi. Hivi ndivyo Haiti, Marekani na Canada zitakavyoshughulikia jambo hili wiki ijayo wakati wa vikao vya ngazi ya juu vya Mkutano mkuu wa Umoja huo. Ecuador pia inaweza kuthibitisha kutuma maafisa wake wa polisi.

Wakati huo huo, mazungumzo ya azimio ambalo lingeunda kikosi hiki yanaendelea. China, ambayo bado ina uhasama na Port-au-Prince kwa kuitambua Taiwan, inalichulia hili kwa shingo upande. Lakini wataalam wa Umoja wa Mataifa wanasalia na matumaini licha ya hayo yote na wanaamini kuwa maazimio hayo yanaweza kupigiwa kura haraka, kabla ya mwisho wa Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.