Pata taarifa kuu
AMANI-USALAMA

Blinken: Mchakato wa kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani Haiti unaendelea

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amekaribisha kuundwa kwa kikosi hiki cha kimataifa katika nchi hii inayokabiliwa na ukosefu wa usalama.

Marekani inataka kusaidia kudumisha amani nchini Haiti kupitia jeshi la kimataifa.
Marekani inataka kusaidia kudumisha amani nchini Haiti kupitia jeshi la kimataifa. © RICHARD PIERRIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema kuridhika Jumamosi hii, Julai 29 na maendeleo yaliyopatikana nchini Haiti kwa ajili ya kuanzishwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani katika nchi hii. Nchi hii ya Amerika ya Kati kwa inakumbwa na ghasia zinazoongezeka pamoja na ukosefu wa usalama.

"Tumedhamiria kuweka kila kitu muhimu kuunda jeshi la kimataifa, ikiwa ni pamoja na kutafuta taifa litakalo simamia kikosi hiki," Blinken amesema. “Ninatumai kuwa hivi karibuni tutaweza kuripoti maendeleo katika eneo hili. Magenge yanadhibiti karibu 80% ya mji mkuu wa Haiti, na uhalifu wa kikatili kama vile utekaji nyara kwa ajili ya fidia, wizi wa kutumia silaha na unyang'anyi wa magari vinaripotiwa mara kwa mara.

Huku vikosi vya usalama vya Haiti vikiwa vimezidiwa nguvu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry wametaka uingiliaji kati wa kimataifa kusaidia polisi. Bwana Guterres ameomba kikosi cha nje kutumwa kwa Umoja wa Mataifa, lakini Baraza la Usalama limemtaka awasilishe, ifikapo katikati ya mwezi wa Agosti, ripoti kuhusu chaguzi zote zinazowezekana, ikiwa ni pamoja na ujumbe ulioelekezwa na Umoja wa Mataifa.

Marekani inawashauri raia wake kutosafiri kwenda Haiti

Nchi kadhaa zimesema zinaunga mkono wazo la jeshi kama hilo, lakini hakuna iliyojitolea kuliongoza. Wiki hii, Marekani iliamuru wafanyikazi wasio wa lazima na familia za maafisa kuondoka Haiti "haraka iwezekanavyo."

Marekani imekuwa ikiwashauri raia wake kutosafiri kwenda Haiti kwa miezi kadhaa, kutokana na hatari ya "utekaji nyara, uhalifu, machafuko ya kiraia na kuharibika kwa miundombinu ya afya". Ushauri wa usafiri, ambao husasishwa mara kwa mara na wizara ya mambo ya nje, unapendekeza kiwango cha usalama cha 4, kiwango cha juu zaidi kutokana na hatari zinazohusika.

Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani tayari wanaishi katika mazingira magumu ya usalama, wamefungwa kwenye eneo la makazi lililohifadhiwa na marufuku kutembea katika mji mkuu au kutumia usafiri wa umma au teksi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.