Pata taarifa kuu
MAREKANI-HAKI

Raia wa Colombia ashtakiwa Marekani kwa kuhusika katika mauaji ya rais wa Haiti

Mwanajeshi wa zamani wa Colombia anakabiliwa na mashitaka nchini Marekani kwa madai ya kushiriki katika mauaji ya rais wa Haiti Jovenel Moïse mwezi Julai mwaka uliyopita, imetangaza Wizara ya Sheria ya Marekani.

Mario Antonio Palacios, 43, raia wa Colombia ambaye alikamatwa na kushtakiwa nchini Marekani kuhusiana na njama ya kumuua Rais wa Haiti Jovenel Moise, amefikishwa mahakamani huko Miami, Florida, Januari 4 2022.
Mario Antonio Palacios, 43, raia wa Colombia ambaye alikamatwa na kushtakiwa nchini Marekani kuhusiana na njama ya kumuua Rais wa Haiti Jovenel Moise, amefikishwa mahakamani huko Miami, Florida, Januari 4 2022. REUTERS - DANIEL PONTET
Matangazo ya kibiashara

Mario Palacios, 43, anatuhumiwa kuwa sehemu ya kundi la watu takriban 20 waliomuua Jovenel Moïse na kumjeruhi vibaya mkewe katika makazi yake huko Port-au-Prince mnamo Julai 7, 2021. Yeye ndiye wa kwanza kushtakiwa kwa kufikishwa mbele ya vyombo vya  sheria vya Marekani kwa mauaji ya rais wa Haiti.

Mario Palacios alikamatwa Jumatatu wiki hii huko Panama wakati ilipotua ndege aliyokuemo kutoka Jamaica, ambapo alikuwa amekimbilia baada ya mauaji, na alikuwa anaelekea nchini Colombia. Alisafirishwa jioni hadi Miami ambapo alifikishwa mahakamani siku ya Jumanne. Anakabiliwa na kifungo cha maisha, wizara ya sheria ilisema kwenye taarifa.

Askari huyo wa zamani wa kikosi maalum cha Colombia aliyeajiriwa mwezi Mei na kampuni ya ulinzi yenye makao yake makuu Miami, kazi yake ya awali ilikuwa kuwalinda watu mashuhuri nchini Haiti. Majukumu yake yalibadilika na kuwa mpango wa kushambulia ikulu ya rais na kumuua rais wa Haiti usiku wa Julai 7. Kundi hilo, chini ya uongozi wa mtu aliyejulikana kama "muandaaji mkuu", lilipewa jukumu la kumuua Jovenel Moïse. Mtu huyu, mwenye uraia pacha wa Haiti na Marekani, yuko kizuizini nchini Haiti.

Mario Palacios tayari amekiri kuwa sehemu ya kundi hilo, kwenye mstari wa mbele kulingana na wachunguzi wa Marekani. amehakikisha kuwa rais alikuwa tayari amefariki alipoingia chumbani kwake. Pia anasema hajui ni nani aliyemuua, ameripoti mwandishi wetu wa Miami, David Thomson. Mario Palacios hata hivyo amekubali kushirikiana na mamlaka za Marekani ambazo zinatumai kwamba ataweza kutoa dalili juu ya kufichuliwa kwa ukweli na juu ya mfadhili wa operesheni hii ambayo inaonekana kuwa iliandaliwa nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.