Pata taarifa kuu
HAITI-HAKI

Haiti: Martine Moïse asikilizwa na jaji kuhusiana na kifo cha mumewe

Ni miezi mitatu sasa Haiti haina rais. Usiku wa Julai 6 kuamkia 7, kundi la watu wenye silaha waliingia katika makazi ya kibinafsi ya Jovenel Moïse na kumuua. Mkewe ambaye alijeruhiwa vibaya na risasi wakati wa shambulio hilo, jana, Jumatano, Oktoba 6, aliitikia mwaliko wa jaji anayehusika na uchunguzi kujibu maswali yake, kama shahidi. Wahusika wa mauaji haya bado hawajatambuliwa.

Martine Moïse wakati wa mazishi ya mumewe aliyeuawa, hayati rais wa Jovenel Moïse, Julai 23, 2021.
Martine Moïse wakati wa mazishi ya mumewe aliyeuawa, hayati rais wa Jovenel Moïse, Julai 23, 2021. Valerie BAERISWYL AFP
Matangazo ya kibiashara

Martine Moïse aliwasili chini ya ulinzi mkali wa polisi katika ofisi ya mwendesha mashtaka wa Port-au-Prince na alikuwa amezungukwa kabisa na walinzi kadhaa wa kigeni waliojihami kwa silaha kali.

Baada ya kusikilizwa kwa zaidi ya masaa matatu katika afisi ya Jaji Garry Orélien, mjane wa Jovenel Moïse aliomba ushiriki mpana katika mchakato huu wa kisheria. “Ninahimiza watu wote kujibu maswali yoyote ambayo yanaweza kuulizwa kutoka kwao. Mtu yeyote aliye na habari: Mjitolee na mjee hapa ili tuweze kusonga mbele na kuwatambua wale waliofanya kitendo hicho kiovu. "

"Ninachotafuta na kusubiri ni haki"

"Ikiwa una habari juu ya mtu ambaye anatafutwa, washirikishe wenzako ili mtu huyo aletwe mbele ya hakimu na uchunguzi unaweza kubaini ikiwa mtu huyo hana hatia au ana hatia, ili tukamilishe kesi hii. Ninachotafuta na kusubiri ni haki, ”aliongeza Martine Moïse.

Mke wa rais aliyeuawa ametangaza kuwa yuko tayari kujibu mwaliko wowote kutoka kwa jaji, bila kujali kesi hiyo. Walakini, hakujibu azma yake ya kuwania kama mgombea katika uchaguzi ujao wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.