Pata taarifa kuu
HAITI

Haiti: Majaji wakataa kuchunguza mauaji ya rais Moïse

Mahakama ya Haiti, kufikia Jumamosi hii Agosti 7, ilikuwa bado haijaanza uchunguzi wake kuhusu mauaji ya rais Jovenel Moïse aliyeuawa na kundi la watu wenye silaha nyumbani kwake.

Watu wakihudhuria mazishi ya rais wa Haiti aliyeuawa Jovenel Moïse Julai 23, 2021, huko Cap-Haitien. - Moïse, 53, aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mapema Julai 7.
Watu wakihudhuria mazishi ya rais wa Haiti aliyeuawa Jovenel Moïse Julai 23, 2021, huko Cap-Haitien. - Moïse, 53, aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mapema Julai 7. AFP - VALERIE BAERISWYL
Matangazo ya kibiashara

Mwezi mmoja baada ya mkasa ambao uliitumbukiza nchi hii katika machafuko, Mkuu wa Mahakama ameshindwa kumpata jaji ambaye yuko tayari kushughulikia kesi hii, ambayo weni wanaona kuwa bomu linalosubiri kulipuka.

"Ni jambo nyeti na la kisiasa. Jaji kabla ya kukubali kuchunguza tukio hilo anafikiria usalama wake na wa familia yake. Hii ndiyo sababu maajaji wanaochunguza kesi kama hizi wana hofu ya kukubali kupewa kusuhulikia kesi hiyo," mmoja wao ameliambia shirika la habari la AFP.

"Majaji kadhaa wanaochunguza kesi kama hizo tayari wamemjulisha mkuu wa mahakama ya mji wa Port-au-Prince kwamba hawapendi kushughulikia kesi hiyo," kimeiongeza chanzo hiki cha mahakama.

Ili kuwahakikishia majaji wake, mkuu wa mahakama hiyo, Bernard Saint-Vil, anasema kuwa ameitaka serikali kutoa ulinzi kwa majaji hao na kuwahakikishia usalama wao.

Kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji ya rais Moïse aliyeuawa Julai 7 nyumbani kwake, polisi wanasema tayari wamewakamata watu 44 wakiwemo polisi 12 wa Haiti, Wacolombia 18 na Wamarekani wawili wenye asili ya Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.