Pata taarifa kuu
HAITI-HAKI

Haiti: Jovenel Moïse kuzikwa Julai 23 Cap, Bertrand Aristide arejea nchini

Mazishi ya rais wa Haiti aliyeuawa kwa kupigwa risasi yatafanyika Julai 23, mamlaka nchini Haiti imetangaza, wakati rais wa zamani wa nchi hiyo Jean-Bertrand Aristide amerudi nyumbani na kulakiwa na wafuasi wake huko Port-au-Prince baada ya kupatiwa matibabu nchini Cuba.

Hayati rais Jovenel Moïse anatarajiwa kuzikwa Julai 23, 2021.
Hayati rais Jovenel Moïse anatarajiwa kuzikwa Julai 23, 2021. REUTERS/Andres Martinez Casares
Matangazo ya kibiashara

Mazishi ya Jovenel Moïse yatafanyika Julai 23 katika mji wa Cap-nchini haiti, serikali imetangaza siku tisa baada ya kuuawa kwa kiongozi huyo nyumbani kwake na kunndi la watu wenye silaha.

Mkewe Martine Moïse, aliyejeruhiwa wakati wa shambulio hilo na kulazwa hospitalini huko Miami, anatarajia kurudi Haiti kuhudhuria mazishi ya mumewe, amesema Kaimu Waziri Mkuu Claude Joseph katika mkutano na waandishi wa habari.

Polisi ya Haiti inawashikilia karibu watu 20, ikiwa ni pamoja na wanajeshi kadhaa wa zamani wa Colombia wanaotuhumiwa kuwa sehemu ya kundi la watu waliokuja kumuua Jovenel Moïse, lakini bado uchunguzi unaendelea.

Polisi ya Colombia, ambayo pia inafanya uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo, siku ya Ijumaa ilisema kwamba afisa wa zamani wa wizara ya sheria ya Haiti, Joseph Felix Badio, aliamuru mamluki wawili wa Colombia wamwue rais Jovenel Moïse.

Watu kadhaa washikiliwa na polisi kwa uchunguzi

Watu hao wenye silaha hapo awali waliagizwa kumkamata Bwana Moïse, alisema Jorge Vargas, mkuu wa polisi wa Colombia, na baadaye maagizo yalibadilishwa, karibu siku tatu kabla ya operesheni hiyo.

Joseph Félix Badio anasakwa na mamlaka ya Haiti, sawa na seneta wa zamani John Joel Joseph, wote wakitajwa kama watu "hatari na wenye silaha".

Vikosi vya usalama vya Colombia, hata hivyo, havikutaja ikiwa Joseph Felix Badio alichukua hatua kwa agizo la wafadhili, wala sababu ambazo zilimfanya atoe agizo hilo.

Mshukiwa mkuu anayedaiwa kuwa mfadhili, Christian Emmanuel Sanon, raia wa Haiti kutoka Florida, alikamatwa Jumapili na polisi wa Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.