Pata taarifa kuu
HAITI

Mauaji ya Jovenel Moïse: "Washukiwa wana uhusiano na mashirika ya Marekani"

Karibu wiki moja baada ya kutangazwa kuuawa kwa rais wa Haiti Jovenel Moïse, maswali mengi juu ya mkasa huu yamekoa majibu. Gotson Pierre, kutoka shirika la mkondoni la Haiti AlterPresse, amezungumzia kuhusu maendeleo ya hivi karibuni katika kesi hii.

Idara ya usalama inasubiri kuwasili kwa ujumbe wa kidiplomasia wa Haiti katika Ubalozi wa Marekani katika eneo la Tabarre, Port-au-Prince, Julai 11, 2021, siku tatu baada ya kuuawa kwa Jovenel Moise.
Idara ya usalama inasubiri kuwasili kwa ujumbe wa kidiplomasia wa Haiti katika Ubalozi wa Marekani katika eneo la Tabarre, Port-au-Prince, Julai 11, 2021, siku tatu baada ya kuuawa kwa Jovenel Moise. Valerie Baeriswyl AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Ni nani aliyemuua rais wa Haiti Jovenel Moïse, au ni nani aliyeamuru mauaji haya? Katika nchi hii ambayo inaendelea kukumbwa na mgogoro wa kisiasa, uchumi, usalama na afya kwa miezi mingi, uvumi umeendelea kusambaa, kujuwa kuna uhusiano gani kati ya watuhumiwa wa mauaji ya rais na Marekani.

RFI imejaribu kumhoji Gotson Pierre kuhusiana na tukio hilo, ili kufahamu zaidi uchunguzi umefikia wapi karibu wiki moja baada ya mauaji ya Jovenel Moïse?

Gotson Pierre amesema: "Hadi sasa, washukiwa 21 wamekamatwa kama sehemu ya uchunguzi, wakiwemo raia 18  wa Colombia- wanajeshi waliostaafu kutoka jeshi la Colombia - na raia watatu wa Haiti. Wacolombia watatu waliuawa na wengine watano bado wako mafichoni".

Mkuu wa usalama wa rais, kamishna wa kitengo Jean Laguel Civil, alikuwa anatarajiwa kusikilizwa na wachunguzi leo Jumanne. Mkuu wa usalama katika ikulu ya rais, Kamishna wa Polisi Dimitri Hérard, anatakiwa kujibu maswali ya wachunguzi Jumatano wiki hii. Hatua zimechukuliwa dhidi yao na nafasi zao zimepewa watu wengine.

Mmoja wa Wamarekani wenye asili ya Haiti waliokamatwa nchini Haiti kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya rais Jovenel Moïse wiki iliyopita alikuwa afisa wa shirika la Marekani la kupambana na biashara ya dawa za kulevya, DEA (Drug Enforcement Administration), mkuu wa shirika hilo amesema.

Mamlaka ya Haiti, wiki iliyopita, iliwakamata Wamarekani wawili wenye asili ya Haiti, Joseph Vincent na James Solages, wanaotuhumiwa kushiriki na raia 26 wa Colombia katika operesheni mbaya dhidi ya rais wa Haiti.

Akiongea kwa sharti la kutotajwa jina, mwakilishi huyo wa DEA alikataa kusema ni yupi kati ya watu hao wawili alikuwa afisa wa shirika hilo la Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.