Pata taarifa kuu
HAITI

Haiti yaomba msaada wa wanajeshi wa Kimataifa

Haiti imetaka vikosi vya kigeni kutumwa nchini humo kulinda miundo mbinu muhimu baada ya kuuawa kwa rais Jovenel Moïse wiki hii.

Maafisa wa usalama nchini Haiti
Maafisa wa usalama nchini Haiti AFP - VALERIE BAERISWYL
Matangazo ya kibiashara

Serikali nchini humo imetoa ombi hilo kwa serikali ya Marekani na Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, Marekani imesema haina mpango wa kutuma wanajeshi wake nchini humo kwa sasa, lakini badala yake itatuma maafisa wa FBI na watalaam wake kusaidia kwenye uchunguzi.

Hii imekuja baada ya polisi wa Haiti kudai kuwa mamluki 28 kutoka nje ya nchi ndio waliomuua rais huyo wa Haiti siku ya Jumatano.

Baada ya makabiliano ya saa kadhaa jijini Port-au-Prince, washukiwa 17 walikamatwa wakiwemo wanajeshi wastaafu kutoka nchini Colombia.

Washukiwa wengine watatu waliuawa na wengine wanane, bado wanatafutwa.

Mauaji ya rais Moise, yamezua hali ya taharuki katika taifa hilo masikini katika bara la America, huku hali ya hatari ikiendelea kushuhudiwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.