Pata taarifa kuu
HAITI-SIASA

Watu wanne wanaohusishwa na kifo cha rais wa Haiti, wauawa

Polisi nchini Haiti, wamewauwa watu wanne, wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha rais wa nchi hiyo Jovenel Moise siku ya Jumatano.

Marehemu Jovenel Moise aliyekuwa rais wa Haiti
Marehemu Jovenel Moise aliyekuwa rais wa Haiti CHANDAN KHANNA AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa wengine wawili wametiwa mbaroni wakati huu viongozi mbalimbali duniani wakilaani kuuawa kwa kiongozi wa nchi hiyo ya eneo la Caribbean.

Mpaka sasa haijafahamika wauaji wa rais huyo walikuwa na nia gani, na ni akina nani.Imeripotiwa kuwa wauaji hao walikuwa wanazungumza lugha ya Kiingereza na Kispanyola.

Mkuu wa jeshi la Polisi Leon Charles amesema msako unaendelea kuwatafuta washukiwa zaidi wa mauaji hayo.

Wakati huu tunapozungumza, polisi wanakabiliwa na washukiwa hao, tunawafuata, tutawauwa au kuwakamata

Bocchit Edmond Balozi wa Haiti nchini Marekani amesema tukio hilo la kusikitisha, linapaswa kuwaunganisha raia wa nchi hiyo.

Baada ya tukio hili la kusikitisha sisi kama viongozi, tunapaswa kuwa na njia ya kuja pamoja, kwa hivyo nafikiri kwa sasa ni kiongozi kukaa na kila mmoja na kutulia suala hilo la  kusikitisha kwa maslahi ya nchi na sio kuigawa nchi zaidi.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limelaani mauaji ya kiongozi huyo na kutaka wale wote waliohusika kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Waziri Mkuu, Claude Joseph ametangaza hali ya dharura na kueleza kuwa kwa sasa yeye ndiye anayeongoza nchi hiyo wakati huu mitaa ya jiji kuu Port-au-Prince, ukisalia bila watu na uwanja wa ndege kufungwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.