Pata taarifa kuu
HAITI-USALAMA

Haiti: Mamia ya wakaazi watoroka makazi yao kufutia mapigano

Mamia ya wakaazi wa eneola Martissant, katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, wameyatoroka makazi yao kufuati mapiano kati ya makundi hasimu yanayopania kudhibiti eno hilo.

Mashirika ya kiraia yanalaani tabia ya serikali kushindwa kuwalinda raia masikini na mapigano chini Haiti.
Mashirika ya kiraia yanalaani tabia ya serikali kushindwa kuwalinda raia masikini na mapigano chini Haiti. AFP - VALERIE BAERISWYL
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa eneo la Martissant wamelazimika kukimbilia haraka maeneo jirani, kwa hofu ya usalama wao kutokana na makabiliano hayo ya makundi hasimu yanayoendelea kwa siku kadhaa.

Zaidi ya watu 560 wamekimbilia katika wilaya jirani la Carrefour,kulinana na vyanzo kutoka polisi. Eneo la Martissant linapatikana mita mia chache tu kutoka ikulu ya rais. Kutokana na kushindwa kwa mamlaka kuzuia mapigano hayo, mashirika ya kiraia yanalaani tabia ya serikali ya kushindwa kutoa ulinzi wa kutosha kwa raia hawa masikini.

"Ni wakazi wote wa maeneo ya Martissant na Fontamara ambao hawawezi kurudi nyumbani na ambao kwamelazimika kukimbilia mahali pa umma au pembeni mwa barabara", amebainisha Marie Rosy Auguste Ducena, kutoka moja ya mashirika yanayotetea haki za binadamu . Hata hivyo amebaini kwamba wakaazi wengine wa eneo la Martissant wamekwama majumbani mwao kwa siku mbili au tatu, bila kuweza kwenda kununua chakula, kwa sababu hawataruhusiwa kuondoka katika eneo hilo.

Watu kadhaa wameuawa, magari na nyumba zilichomwa moto, lakini idadi kamili ya vifo au majeruhi kati ya makundi hayo hasimu bado haijajulikana. Bado ni vigumu kufika katika eneo hilo mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.